-
Pigano la Biblia ya Kifaransa la KuokokaAmkeni!—1997 | Desemba 8
-
-
Baadaye, kanisa lililaumu Waldo na wafuasi wake likiwaita wazushi, na watawa wa kiume wakachoma tafsiri alizokuwa ameagiza. Kuanzia hapo na kuendelea, kanisa lilikinza kila jitihada ya kufanya Neno la Mungu lipatikane mikononi mwa watu wa kawaida.
Kanisa lilidhihirisha hila yake mwaka wa 1211 kwa kuchoma Biblia katika jiji la Metz, mashariki ya Ufaransa. Mwaka wa 1229 Baraza la Toulouse lilikataza kabisa watu wa kawaida kutumia Biblia za lugha za wenyeji katika lugha yoyote ile. Hilo lilifuatwa mwaka wa 1234 na Baraza la Tarragona, Hispania, ambalo lilikataza mtu kuwa na Biblia katika yoyote ya lugha za Kiroma (lugha zilizotokana na Kilatini), hata na makasisi.
-
-
Pigano la Biblia ya Kifaransa la KuokokaAmkeni!—1997 | Desemba 8
-
-
Pigano Lenye Hatari
Katika Ufaransa baadhi ya wachapaji jasiri kama Étienne Dolet katika mwaka wa 1546, walichomwa mtini kwa sababu ya kuchapa Biblia. Baraza la Trent, katika mwaka wa 1546, lilihakikisha “uasilia” wa Vulgate, yajapokuwa makosa yake, na tangu wakati huo na kuendelea kanisa lilichukua msimamo uliozidi kuimarika dhidi ya tafsiri za lugha ya wenyeji. Mwaka wa 1612 Baraza la Kuhukumu Wazushi la Hispania lilianzisha kampeni kali ya kukomesha Biblia za lugha ya wenyeji.
Nyakati nyingine mnyanyaso uliongoza kwenye uvumbuzi mnyoofu. “Msokoto wa nywele,” au “fundo la nywele,” Biblia zilikuwa zikitokezwa, ambazo zilikuwa na udogo wa kutosha kufichwa katika fundo la nywele za mwanamke. Na mwaka wa 1754, madondoo ya Maandiko ya Kiebrania na Kigiriki yalichapwa katika kitabu kilichokuwa na kipimo cha sentimeta tatu kwa tano tu.
-
-
Pigano la Biblia ya Kifaransa la KuokokaAmkeni!—1997 | Desemba 8
-
-
Kanisa Katoliki lilikinza badiliko lolote katika mbinu zake, lakini lilikuwa linashindwa. Katika karne yote ya 19, mapapa walitoa mfululizo wa maagizo yakipinga kikatili Biblia za lugha ya wenyeji. Kufikia mwisho-mwisho wa 1897, Papa Leo wa 13 alisisitiza tena kwamba “tafsiri zote za Vitabu Vitakatifu zilizofanyizwa na mwandikaji yeyote yule asiye Mkatoliki na kwa lugha yoyote ya kawaida zimekatazwa, hasa zile zilizochapishwa na sosaiti za Biblia, ambazo zimelaumiwa na Papa wa Roma mara kadhaa.”
-