Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
    • Barabara ya Via Appia iliitwa kwa jina la ofisa fulani Mroma (Appius Claudius Caecus), aliyeanza kuijenga mwaka wa 312 K.W.K. Barabara hiyo yenye upana wa mita 5 hadi 6, imefunikwa kwa mawe makubwa ya volkano. Barabara ya Via Appia, yenye urefu wa kilomita 583, iliunganisha Roma na bandari ya Brundisium (Brindisi ya siku hizi), upande wa kusini-mashariki. Hapo ndipo safari za kwenda Mashariki zilianzia siku za kale. Wasafiri walikatiza safari zao kwenye vituo mbalimbali vya kupumzikia vilivyopatikana baada ya kila kilomita 24 hivi. Katika vituo hivyo waliweza kununua bidhaa, kulala, au kubadilisha farasi au magari yaliyokokotwa na farasi.

      Yaelekea Paulo, alipokuwa njiani kwenda Roma, alitembea kwa miguu kwa umbali wa kilomita 212 hivi kwenye barabara ya Via Appia. Alivuka eneo lenye majimaji la Pontine katika safari hiyo. Mwandikaji mmoja Mroma alilalamika kuhusu mbu wengi na harufu mbaya sana ya eneo hilo. Soko la Apio lilikuwa kaskazini ya eneo hilo, umbali wa kilomita 70 hivi kutoka Roma. Kituo cha kupumzikia cha Mikahawa Mitatu kilikuwa umbali wa kilomita 50 hivi kutoka jiji hilo.

  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi—2010 | Januari 1
    • [Picha katika ukurasa wa 11]

      Via Appia

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki