Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Opera—Katika Msitu
    Amkeni!—1997 | Mei 22
    • Katika 1923, hali ya Brazili ya kudhibiti mpira ilianguka. Kwa kasi sana, makabaila, wabashiri wa mambo ya kifedha, wafanyabiashara, na makahaba wakahama mji huo, likifanya Manaus kuwa mwitu wenye magugu tu. Na vipi jumba la opera? Vyumba vya ziada vikawa bohari za mpira, na jukwaa likawa uwanja wa kandanda unaochezwa ndani ya jumba!

  • Opera—Katika Msitu
    Amkeni!—1997 | Mei 22
    • Utekwa Ulioangamiza Biashara ya Mpira na Kukomesha Jumba la Opera

      Katika 1876, Henry Wickham, mjasiri mmoja mchanga wa Uingereza, alifanya njama ambayo iliangamiza biashara yenye kunawiri ya mpira. Kwa msaada wa Wahindi, yeye “aliteka” mbegu bora 70,000 aina ya Hevea brasiliensis zilizokusanywa katika msitu wa Amazon, akazipakia kwenye meli, na kuzipitisha kiharamu katika forodha ya Brazili kwa kisingizio cha kwamba hizo ni “sampuli za mimea nadra sana zilizokuwa zikipelekewa Malkia Victoria.” Alizitunza katika mashua akivuka Atlantiki na kuzipeleka mbio kwa gari-moshi lililokodishwa hadi kwenye mabanda ya kukuzia mimea ya Royal Botanic Gardens kule Kew, Uingereza, ambako mbegu zilichipuka majuma machache baadaye. Kutoka huko, zilisafirishwa hadi Asia na kupandwa katika ardhi ya mabwawa ya Ceylon na Peninsula ya Malay. Kufikia 1912, mbegu hizo zilizotekwa zilikuwa zimekuwa mashamba ya mipira isiyoweza kushikwa na maradhi, na kufikia wakati miti hiyo iliweza kutokeza utomvu, chasema chanzo kimoja cha habari, “unawiri wa biashara ya mpira ya Brazili [ulikuwa umeanguka] kabisa.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki