Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nunua Dhahabu Iliyosafishwa kwa Moto
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 12. Ni nani aliyekuwa mmoja wa wale waliokuwa wakichukua uongozi miongoni mwa Wakristo waliokuwa wakiamka, naye aliwekaje kielelezo chenye kutokeza katika kujiwekea hazina katika mbingu?

      12 Charles Taze Russell ndiye aliyekuwa akichukua uongozi miongoni mwa Wakristo hawa waliokuwa wakiamka, na ambaye, mapema katika miaka ya 1870, alianzisha darasa la kujifunza Biblia katika Allegheny (sasa ni sehemu ya Pittsburgh), Pennsylvania, U.S.A. Alipoanza utafutaji wake wa ukweli, Russell alikuwa katika biashara-shirika pamoja na baba yake na alikuwa akielekea kuwa milionea. Lakini yeye aliuza faida za biashara yake ya duka moja baada ya jingine na kutumia utajiri wake katika kusaidia kifedha kazi ya kuhubiri Ufalme wa Mungu katika dunia yote. Katika 1884 Russell akawa msimamizi wa kwanza wa lile shirika linalojulikana sasa kuwa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania. Katika 1916 yeye alikufa akiwa ndani ya garimoshi karibu na Pampa, Teksasi, njiani kwenda New York, akiwa amemalizwa nguvu kabisa na safari yake ya mwisho ya kuhubiri magharibi mwa United States. Yeye aliweka kielelezo chenye kutokeza cha kujiwekea hazina za kiroho katika mbingu, kielelezo ambacho leo kinafuatwa na mamia ya maelfu ya wahudumu mapainia wenye kujidhabihu.—Waebrania 13:7; Luka 12:33, 34; linga 1 Wakorintho 9:16; 11:1.

  • Nunua Dhahabu Iliyosafishwa kwa Moto
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika 1879 Pasta Russell, kama alivyoitwa kwa shauku ya upendo, alianza kutangaza kwa kuutetea ukweli gazeti linalojulikana ulimwenguni pote leo kuwa Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova. Katika toleo lalo la pili, yeye alitangaza hivi: “Tunaitikadi kwamba [Gazeti hili] lina YEHOVA akiwa mtegemezaji walo, na maadamu ndivyo ilivyo halitaomba-omba kamwe wala kuomba rasmi wanadamu kwa ajili ya kusaidiwa. Wakati Yeye anayesema: ‘Dhahabu yote na fedha yote ya milimani ni zangu,’ anashindwa kutoa pesa zinazohitajiwa, sisi tutaelewa kuwa ni wakati wa kusimamisha uchapaji.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki