Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutetea Imani Yetu
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Desemba 1
    • b Baada ya makala hiyo yenye uchongezi kuchapishwa katika gazeti la habari la Urusi (lililotajwa katika fungu la 15), Mashahidi wa Yehova walikata rufani kwa baraza la sheria liitwalo Russian Federation Presidential Judicial Chamber for Media Disputes wakiomba mashtaka hayo yasiyo ya kweli ambayo yaliandikwa katika makala hiyo yachunguzwe tena. Hivi majuzi mahakama ilitoa uamuzi ulioliadhibu vikali gazeti hilo la habari kwa kuchapa makala hiyo yenye kukashifu.—Ona Amkeni!, Novemba 22, 1998, ukurasa wa 26-27.

  • Kutetea Imani Yetu
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Desemba 1
    • Kwa kielelezo, Agosti 1, 1997, gazeti la habari la Urusi lilichapisha makala yenye uchongezi iliyodai kwamba, kati ya mambo mengine, Mashahidi kwa hakika huwataka washiriki wao ‘wakatae wake zao, waume wao, na wazazi wao iwapo hawaelewi na iwapo imani yao ni tofauti na yao.’ Mtu yeyote anayewafahamu Mashahidi wa Yehova kikweli anajua kwamba shtaka hilo si la kweli. Biblia huonyesha kwamba Wakristo wapaswa kuwatendea washiriki wa familia wasioamini kwa upendo na staha, nao Mashahidi hujitahidi sana kufuata mwelekezo huo. (1 Wakorintho 7:12-16; 1 Petro 3:1-4) Hata hivyo, makala hiyo ilichapwa, na hivyo wasomaji wengi wakapotoshwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki