-
Urusi2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Jua linapotua kwa watumishi washikamanifu wa Yehova katika jiji la Kaliningrad lililo magharibi mwa Urusi, tayari wahubiri wanaoishi kwenye Rasi ya Chukchi, ambayo iko kwenye Mlango-Bahari wa Bering unaotenganisha rasi hiyo na Alaska, huliona likichomoza.
-
-
Urusi2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Urusi, ambayo sasa inaitwa “Shirikisho la Urusi,” si nchi ya taifa moja au jamii moja. Kama jina lake linavyoonyesha, ni shirikisho la mataifa, mchanganyiko wa makabila, lugha, na jamii nyingi, kila moja ikiwa na utamaduni wake wa pekee. Masimulizi yetu hayaanzi katika demokrasia ya Urusi ya leo bali katika Milki ya Urusi yenye mchanganyiko wa makabila, lugha, na dini nyingi, iliyokuwapo zaidi ya miaka 100 iliyopita ambayo ilitawaliwa na maliki.
-