Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jinsi Dini Ilivyookoka Mashambulizi
    Amkeni!—2001 | Aprili 22
    • “Kanisa Lilithaminiwa Sana na KGB”

      Kanisa Othodoksi liliwasaidia sana Wakomunisti hata baada ya Vita ya Ulimwengu ya Pili kukoma mwaka wa 1945. Kichapo The Soviet Union: The Fifty Years, kilichohaririwa na Harrison Salisbury, kilieleza jinsi ilivyokuwa: “Baada ya vita kukoma, viongozi wa kanisa waliunga mkono madai ya Stalin kuhusu sera ya nchi za kigeni wakati wa Vita Baridi.”

      Kitabu kilichoandikwa hivi karibuni cha The Sword and the Shield chaeleza jinsi viongozi wa kanisa walivyoendeleza masilahi ya Sovieti. Chaeleza kwamba Kiongozi wa Kanisa Alexis wa Kwanza, aliyechukua cheo cha Sergius mwaka wa 1945, “alijiunga na Baraza la Kuleta Amani Duniani, chama cha Sovieti kilichoanzishwa mwaka wa 1949.” Kitabu hicho pia chasema kwamba yeye pamoja na Askofu Mkuu Nikolai “walithaminiwa sana na wapelelezi wa KGB [Halmashauri ya Usalama wa Kitaifa ya Sovieti] kuwa watu waliosaidia serikali kutekeleza malengo yake.”

      Jambo la ajabu ni kwamba mwaka wa 1955, Kiongozi wa Kanisa, Alexis wa Kwanza alitangaza hivi: “Kanisa Othodoksi la Urusi linaunga mkono kikamili sera ya amani ya serikali yetu, si kwa sababu Kanisa halina uhuru, bali kwa sababu sera ya Sovieti ni ya haki na inapatana na mafundisho ya Kikristo yanayohubiriwa na Kanisa.”

      Katika toleo la Januari 22, 2000, la gazeti The Guardian la London, Uingereza, kasisi mpinzani wa Othodoksi Georgi Edelshtein alisema: “Maaskofu wote waliteuliwa kwa uangalifu ili waweze kushirikiana na serikali ya sovieti. Wote walikuwa wapelelezi wa KGB. Inajulikana kote kwamba Kiongozi wa Kanisa Alexy aliyeajiriwa na shirika la KGB, alibandikwa jina la siri la Drozdov. Leo, maaskofu hao wana siasa zilezile walizokuwa nazo miaka 20 au 30 iliyopita.”

  • Jinsi Dini Ilivyookoka Mashambulizi
    Amkeni!—2001 | Aprili 22
    • Taasisi ya Keston ilichunguza kindani ushirikiano kati ya Wasovieti na Alexis wa Pili, ambaye ni kiongozi wa Kanisa Othodoksi la Urusi leo. Ripoti yake ilimalizia hivi: “Ushirikiano wa Aleksi haushangazi kwani karibu viongozi wa dini zote zilizosajiliwa—kutia ndani Wakatoliki, Wabaptisti, Waadventisti, Waislamu na Wabudha—walikuwa vibaraka wa KGB. Hata, ripoti ya kila mwaka inayoeleza ushirikiano wa Aleksi na KGB inataja pia vibaraka wengine wengi, baadhi yao walikuwa viongozi wa Kanisa la Kilutheri la Estonia.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki