Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wakati wa Kutahini (1914-1918)
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 69]

      ‘Hakuna Wanadamu Duniani Waliopendelewa Zaidi’

      Juni 21, 1918, J. F. Rutherford na washirika wake kadhaa wa karibu walihukumiwa kifungo cha miaka 20, wakiwa wamepatikana na hatia bandia ya kufanya njama. Hisia zao zilikuwa nini? Katika barua iliyoandikwa kwa mkono yenye tarehe ya Juni 22-23 (inayoonyeshwa chini), akiwa katika jela kwenye Raymond Street katika Brooklyn, New York, Ndugu Rutherford aliandika: “Labda hakuna wanadamu duniani leo waliopendelewa zaidi na walio na furaha zaidi ya wale ndugu saba walio gerezani sasa. Wao wanajua hawana hatia kabisa ya kosa la kukusudia, na washangilia kuwa wakiteseka pamoja na Kristo kwa ajili ya kumtumikia Yeye kwa uaminifu-mshikamanifu.”

  • Wakati wa Kutahini (1914-1918)
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Picha katika ukurasa wa 69]

      Jela katika Raymond Street, katika Brooklyn, New York, ambamo Ndugu Rutherford na washirika wake kadhaa wa karibu walifungiwa kwa siku saba mara tu baada ya kuhukumiwa kwao

  • Wakati wa Kutahini (1914-1918)
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika masika ya 1918, wimbi la mnyanyaso lilianzishwa dhidi ya Wanafunzi wa Biblia katika Amerika Kaskazini na Ulaya pia. Upinzani huo wenye kuchochewa na makasisi ulifikia upeo katika Mei 7, 1918, wakati waranti za serikali ya muungano ya Marekani zilipotolewa ili kukamata J. F. Rutherford na washirika wake kadhaa wa karibu. Kufikia katikati ya 1918, Rutherford na washirika saba walijipata wakiwa katika gereza la serikali ya muungano katika Atlanta, Georgia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki