Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Lazima Mwe Watakatifu kwa Kuwa Mimi ni Mtakatifu’
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 1
    • 6. Wayahudi katika siku ya Malaki waliitendeaje meza ya Yehova?

      6 Chuki hiyo ilitolewa kielezi kwa wazi Waisraeli walipokuwa wakileta hekaluni kwa mioyo nusu-nusu dhabihu duni, zenye kasoro. Kupitia nabii wake Malaki, Yehova alishutumu matoleo yao hafifu: “Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu. . . . Lakini ninyi mnalitia unajisi, kwa kuwa mwasema, Meza ya BWANA imetiwa unajisi; na matunda yake, yaani, nyama yake, hudharauliwa. Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! niikubali hii mikononi mwenu? asema BWANA.”—Malaki 1:10, 12, 13.

  • Lazima Mwe Watakatifu kwa Kuwa Mimi ni Mtakatifu’
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Agosti 1
    • 9, 10. Tufikirieje kumwabudu kwetu Yehova?

      9 Kama tulivyoona awali, kwa sababu ya ile hali mbaya ya kiroho katika siku ya Malaki, Yehova alilaumu waziwazi ibada ya kijuujuu ya Yuda naye akaonyesha kwamba angekubali ibada safi pekee. Je, hilo halipaswi kutufanya tufikirie ubora wa ibada yetu kwa Yehova Mungu, Bwana Mwenye Enzi Kuu wa ulimwengu wote mzima, Chanzo cha utakatifu wa kweli? Je, kwa kweli twamtolea Mungu utumishi mtakatifu? Je, tunajiweka wenyewe katika hali iliyo safi kiroho?

      10 Hilo halimaanishi kwamba twapaswa kuwa wakamilifu, jambo ambalo haliwezekani, au kwamba twapaswa kujilinganisha na wengine. Lakini hilo humaanisha kwamba kila Mkristo apaswa kuwa akimtolea Mungu ibada iliyo bora zaidi kulingana na hali zake. Hilo hurejezea ubora wa ibada yetu. Utumishi wetu mtakatifu wapaswa kuwa ulio bora zaidi—utumishi mtakatifu. Hilo hutimizwaje?—Luka 16:10; Wagalatia 6:3, 4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki