Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dhabihu Zilizompendeza Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Agosti 15
    • 16. (a) Kusudi la toleo la dhambi na toleo la hatia lilikuwa nini? (b) Matoleo hayo yalitofautianaje na toleo la kuchomwa?

      16 Dhabihu zilizotolewa ili kutafuta msamaha wa dhambi au kufunika ukiukaji wa Sheria zilitia ndani toleo la dhambi na toleo la hatia. Ingawa dhabihu hizi zilichomwa kwenye madhabahu, zilikuwa tofauti na toleo la kuchomwa kwa kuwa mafuta na sehemu fulani za mnyama ndizo zilizotolewa kwa Mungu, bali si mnyama mzima. Mabaki ya mnyama huyo yalitupwa nje ya kambi au wakati mwingine yaliliwa na makuhani. Tofauti hiyo ni muhimu. Toleo la kuchomwa lilikuwa zawadi kwa Mungu ili kufanya iwezekane kumkaribia, hivyo toleo lote lilitolewa kwa Mungu peke yake. Jambo la kutokeza ni kwamba toleo la dhambi au toleo la hatia lilitangulia toleo la kuchomwa, ikidokeza kwamba msamaha wa dhambi ulihitajika ili zawadi ya mtenda-dhambi ikubalike kwa Mungu.—Mambo ya Walawi 8:14, 18; 9:2, 3; 16:3, 5.

  • Dhabihu Zilizompendeza Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Agosti 15
    • 18 Maana na kusudi la toleo la hatia zafafanuliwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi sura ya 5 na 6. Huenda mtu akawa alifanya dhambi bila kukusudia. Hata hivyo, huenda ikawa dhambi yake ilimfanya awe na hatia ya kuvunja haki za wanadamu wenzake au za Yehova Mungu, kosa lililopasa kulipizwa au kusahihishwa. Aina kadhaa za dhambi zinatajwa. Baadhi ya dhambi hizo zilikuwa za faragha (5:2-6), nyingine zilikuwa dhambi dhidi ya “mambo matakatifu ya BWANA” (5:14-16), na nyingine, japo kwa kadiri fulani zilikuwa za kukusudia, zilikuwa dhambi zilizotokana na tamaa mbaya au udhaifu wa mwili (6:1-3). Mbali na kutubu dhambi hizo, mkosaji alitakiwa kutoa fidia ikihitajika kisha kutoa toleo la hatia kwa Yehova.—Mambo ya Walawi 6:4-7.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki