Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dhabihu Zilizompendeza Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Agosti 15
    • 13. Fafanua matoleo yaliyotolewa kwa hiari yakiwa zawadi kwa Mungu.

      13 Matoleo ya kuchomwa, matoleo ya nafaka, na matoleo ya ushirika ni kati ya matoleo yaliyotolewa kwa hiari yakiwa zawadi au njia ya kumkaribia Mungu ili kupata kibali chake.

  • Dhabihu Zilizompendeza Mungu
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Agosti 15
    • 15. Dhabihu ya ushirika ilitolewa kwa kusudi gani?

      15 Toleo jingine la hiari lilikuwa dhabihu ya ushirika, ambayo yafafanuliwa katika kitabu cha Mambo ya Walawi sura ya 3. Dhabihu ya ushirika yaweza pia kutafsiriwa kuwa “dhabihu ya matoleo ya amani.” Katika Kiebrania, neno “amani” lamaanisha mengi zaidi ya kutokuwa na vita au machafuko. “Katika Biblia, lamaanisha hivyo, na pia lamaanisha hali au uhusiano wenye amani pamoja na Mungu, ufanisi, shangwe, na furaha,” chasema kitabu Studies in the Mosaic Institutions. Hivyo, dhabihu za ushirika zilitolewa si kwa ajili ya kupata amani pamoja na Mungu, kana kwamba kumtuliza, bali ili kushukuru au kusherehekea kwa sababu ya hali nzuri ya amani pamoja na Mungu ambayo hufurahiwa na wale wanaokubaliwa naye. Makuhani na mtoaji walikula dhabihu baada ya kumtolea Yehova damu na mafuta. (Mambo ya Walawi 3:17; 7:16-21; 19:5-8) Katika njia ya mfano na yenye kupendeza, mtoaji, makuhani, na Yehova Mungu walikuwa kana kwamba wanakula pamoja, hilo likionyesha uhusiano wenye amani uliokuwepo miongoni mwao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki