-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha Pili cha SamweliMnara wa Mlinzi—2005 | Mei 15
-
-
DAUDI AWA “MKUU ZAIDI NA ZAIDI”
Itikio la Daudi anapopata habari za kifo cha Sauli na Yonathani linaonyesha hisia zake kuwaelekea na kumwelekea Yehova. Huko Hebroni, Daudi anawekwa kuwa mfalme wa kabila la Yuda, naye Ish-boshethi, mwana wa Sauli, anawekwa kuwa mfalme wa yale makabila mengine ya Israeli. Daudi ‘anaendelea kuwa mkuu zaidi na zaidi,’ na miaka saba na nusu hivi baadaye, anafanywa kuwa mfalme wa taifa lote la Israeli.—2 Samweli 5:10.
Daudi anateka Yerusalemu kutoka kwa Wayebusi na kuufanya mji mkuu wa ufalme wake. Jaribio lake la kwanza la kulihamisha sanduku la agano hadi Yerusalemu linatokeza msiba. Lakini, jaribio la pili linafanikiwa, na Daudi anacheza dansi kwa furaha. Yehova anafanya agano pamoja na Daudi kwa ajili ya ufalme. Daudi anawatiisha adui zake, na Mungu anaendelea kuwa pamoja naye.
-
-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha Pili cha SamweliMnara wa Mlinzi—2005 | Mei 15
-
-
YEHOVA ALETA MSIBA DHIDI YA MTIWA-MAFUTA WAKE
Yehova anamwambia Daudi hivi: “Tazama, ninaleta msiba juu yako kutoka katika nyumba yako mwenyewe; nami nitawachukua wake zako chini ya macho yako mwenyewe na kumpa mwanamume mwenzako, naye atalala na wake zako chini ya macho ya jua hili.” (2 Samweli 12:11) Kwa nini Yehova anasema hivyo? Kwa sababu ya dhambi ya Daudi na Bath-sheba. Ingawa Daudi anasamehewa baada ya kutubu, haepuki matokeo ya dhambi yake.
Kwanza, mtoto ambaye Bath-sheba anazaa anakufa. Kisha, Tamari, binti ya Daudi, ambaye ni bikira, analalwa kinguvu na Amnoni, ndugu yake wa kambo. Absalomu, ndugu ya Tamari, analipiza kisasi kwa kumuua Amnoni. Absalomu anapanga njama dhidi ya babake na kujitangaza kuwa mfalme huko Hebroni. Daudi analazimika kukimbia Yerusalemu. Absalomu analala na masuria kumi wa babake wanaoachwa nyuma kutunza nyumba. Daudi anaurudia utawala wake baada ya Absalomu kuuawa. Uasi unaoanzishwa na Sheba, Mbenyamini, unasababisha kifo chake.
-
-
Mambo Makuu Katika Kitabu cha Pili cha SamweliMnara wa Mlinzi—2005 | Mei 15
-
-
ACHA TUANGUKE “MKONONI MWA YEHOVA”
Kunakuwa na njaa kwa miaka mitatu kwa sababu ya hatia ya Sauli ya kumwaga damu kwa kuwaua Wagibeoni. (Yoshua 9:15) Ili kulipiza kisasi, Wagibeoni wanaomba wapewe wana saba wa Sauli ili wawaue. Daudi anawapa wana hao, mvua inanyesha, na ukame unaisha. Majitu wanne Wafilisti ‘wanaanguka kwa mkono wa Daudi na kwa mkono wa watumishi wake.’—2 Samweli 21:22.
Daudi anafanya dhambi nzito kwa kuagiza watu wahesabiwe isivyo halali. Anatubu na kuchagua kuanguka “mkononi mwa Yehova.” (2 Samweli 24:14) Kwa hiyo, watu 70,000 wanakufa kutokana na tauni. Daudi anafuata amri ya Yehova, na tauni inakomeshwa.
-