Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nguvu za Kuumba—“Aliyezifanya Mbingu na Nchi”
    Mkaribie Yehova
    • 6. Biblia inaonyeshaje kwamba idadi ya nyota ni kubwa sana wanadamu wasiweze kuhesabu?

      6 Lakini idadi ya nyota inastaajabisha zaidi ya ukubwa wake. Kwa kweli, Biblia inasema kwamba nyota haziwezi kuhesabiwa, kama vile “mchanga wa bahari” usivyoweza kuhesabiwa. (Yeremia 33:22) Maneno hayo yanadokeza kwamba kuna nyota nyingi sana ambazo hatuwezi kuona pasipo vifaa maalumu. Endapo mwandikaji wa Biblia, kama Yeremia, angetazama angani wakati wa usiku na kujaribu kuhesabu nyota zionekanazo, angefaulu kuhesabu nyota zipatazo 3,000 hivi. Wanadamu huweza kuona idadi hiyo tu ya nyota katika anga jangavu la usiku bila kutumia vifaa maalumu. Idadi hiyo yaweza kulinganishwa na idadi ya chembe za mchanga zinazoweza kujaza kiganja kimoja tu cha mkono. Hata hivyo, idadi halisi ya nyota haijulikani, ni nyingi kama mchanga wa bahari. Ni nani awezaye kuhesabu idadi kubwa hivyo?b

      Nyota nyingi sana za mbinguni na makundi ya nyota

      “Aziita zote kwa majina”

      7. (a) Kundi letu la Kilimia lina nyota ngapi, na hiyo ni idadi kubwa kadiri gani? (b) Kushindwa kwa wataalamu wa nyota kuhesabu makundi ya nyota kwaonyesha nini, na hilo latufundisha nini kuhusu nguvu za Yehova za kuumba?

      7 Andiko la Isaya 40:26 linajibu hivi: “Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina.” Zaburi 147:4 yasema: “Huihesabu idadi ya nyota.” “Idadi ya nyota” ni ngapi? Hilo si swali rahisi. Wataalamu wa nyota wanakadiria kwamba kuna zaidi ya nyota bilioni 100 katika kundi letu la nyota la Kilimia peke yake. Lakini kuna makundi mengine mengi mbali na kundi letu, ambayo yana nyota nyingi zaidi. Kuna makundi mangapi? Baadhi ya wataalamu wa nyota wamekadiria kwamba kuna makundi bilioni 50. Wengine wamekadiria kwamba kuna makundi yapatayo bilioni 125. Kwa hiyo, mwanadamu hawezi hata kujua idadi ya makundi ya nyota, sembuse kujua idadi kamili ya mabilioni ya nyota zilizomo.

  • Nguvu za Kuumba—“Aliyezifanya Mbingu na Nchi”
    Mkaribie Yehova
    • b Watu fulani hufikiri kwamba watu walioishi katika nyakati za Biblia walitumia darubini fulani ya kienyeji. Wanatoa sababu kwamba watu walioishi nyakati hizo hawangeweza kujua kwamba idadi ya nyota ni kubwa sana wanadamu wasiweze kuhesabu. Makisio hayo yasiyo na msingi hayamheshimu wala kumtambua Yehova, Mtungaji wa Biblia.—2 Timotheo 3:16.

      c Fikiria muda ambao ungehitaji kutumia kuhesabu nyota bilioni 100 tu. Kama ungeweza kuhesabu nyota moja kila sekunde—kwa muda wa saa 24 kwa siku—ingekuchukua miaka 3,171!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki