Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siku ya Hukumu ya Mungu—Matokeo Yayo Yenye Shangwe!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 16. (a) Ni majina ya nani ambayo hayataandikwa katika hati-kunjo, au kitabu, ya uhai? (b) Ni nani wale ambao ufufuo wao utathibitika kuwa “wa uhai”?

      16 Kwa habari ya ufufuo wa kidunia, Yesu alisema kwamba ‘wale waliofanya mema hutoka na kuja kwenye ufufuo wa uhai, wale waliozoea vitu vibaya sana kwenye ufufuo wa hukumu.’ Hapa “uhai” na “hukumu” hutofautiana, kuonyesha kwamba wale wafufuliwa ambao ‘huzoea vitu vibaya sana’ baada ya kufundishwa katika Maandiko na hati-kunjo zilizovuviwa huhukumiwa kuwa hawastahili uhai. Majina yao hayataandikwa katika hati-kunjo au kitabu, ya uhai. (Yohana 5:29, NW) Inaweza kuwa hivyo pia kwa wowote ambao hapo kwanza walifuata mwendo wa uaminifu lakini ambao, kwa sababu fulani, wanakengeuka katika wakati wa Utawala wa Miaka Elfu. Majina yanaweza kufutwa. (Kutoka 32:32, 33)

  • Siku ya Hukumu ya Mungu—Matokeo Yayo Yenye Shangwe!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kwa wazi ni hapa mwishoni mwa miaka elfu, ndipo Shetani anaachiliwa na mtihani wa mwisho kabisa unafanyika kuamua ni majina ya nani yatabaki daima yamerekodiwa katika hati-kunjo ya uhai. “Jitahidini wenyewe kisulubu” ili jina lenu liwe miongoni mwayo!—Luka 13:24; Ufunuo 20:5, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki