Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 21. Kunakuwa nini wakati malaika wa pili anapopuliza tarumbeta yake?

      21 “Na malaika wa pili akapuliza tarumbeta yake. Na kitu fulani kama mlima mkubwa unaowaka moto kilivurumishwa ndani ya bahari. Na theluthi moja ya bahari ikawa damu; na theluthi moja ya viumbe ambao wamo ndani ya bahari ambao wana nafsi wakafa, na theluthi moja ya mashua zikaharibiwa.” (Ufunuo 8:8, 9, NW)

  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Lakini waovu ni kama bahari ambayo inarushwarushwa, wakati inapokuwa haiwezi kutulia, maji yayo ambayo huendelea kurusharusha juu magugubahari na topetope.” (Isaya 57:20; 17:12, 13, NW) Hivyo, “bahari” hutoa vizuri picha ya binadamu wasiopumzika, wasiotulia, na wenye uasi wanaochochea kutopumzika na mapinduzi. (Linga Ufunuo 13:1.) Utakuja wakati ambapo hiyo “bahari” itakuwa haipo tena. (Ufunuo 21:1) Lakini kwa wakati uliopo, kwa mpigo wa tarumbeta ya pili, Yehova anatamka hukumu dhidi ya “theluthi moja” yayo—ile sehemu yenye utukutu iliyo katika milki ya Jumuiya ya Wakristo yenyewe.

  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 27. (a) “Theluthi moja ya bahari” imekuwaje kama damu? (b) ‘Theluthi moja ya viumbe katika bahari’ walikufaje na itakuwaje kwa “theluthi moja ya mashua”?

      27 Ule mpigo wa pili wa tarumbeta hufunua kwamba wale wa aina ya binadamu ambao walijihusisha katika mipambano ya kimapinduzi juu ya serikali badala ya kujitiisha kwenye Ufalme wa Mungu ni wenye hatia ya damu. Hasa “theluthi ya bahari” ya Jumuiya ya Wakristo imekuwa kama damu. Vitu vyote vilivyo hai humo ni vifu machoni pa Mungu. Hakuna yoyote ya yale matengenezo ya kisoshalisti yanayoelea kama mashua katika theluthi hiyo ya bahari yanaweza kuepuka mvunjikomeli wa mwisho kabisa. Jinsi sisi tulivyo wenye furaha kwamba mamilioni ya watu wenye mfano wa kondoo sasa wametii mwito kama wa tarumbeta wajitenge na wale ambao wangali wanagaagaa katika utukuzo wa taifa usio na akili na hatia ya damu ya bahari hiyo!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki