-
Alizeti—Ua Maridadi na Lenye ManufaaAmkeni!—2005 | Agosti 22
-
-
Lakini kufikia katikati ya karne ya 18, mbegu za alizeti zilianza kuliwa.
-
-
Alizeti—Ua Maridadi na Lenye ManufaaAmkeni!—2005 | Agosti 22
-
-
Shina gumu na majani ya kijani yasiyo laini hufunikwa na ua kubwa lenye umbo la duara na petali za manjano. Petali hizo huzunguka eneo jeusi la katikati lililo na maua madogo yenye mirija. Maua hayo madogo yakichavushwa na wadudu, husitawi na kuwa mbegu ndogo za alizeti ambazo huliwa. Sehemu hiyo ya katikati ya alizeti inaweza kuwa na kipenyo cha kati ya sentimeta 5 na 50, na hutokeza mbegu 100 hadi 8,000 hivi.
-
-
Alizeti—Ua Maridadi na Lenye ManufaaAmkeni!—2005 | Agosti 22
-
-
Leo, alizeti hupandwa kwa wingi hasa kwa sababu mbegu zake hutokeza mafuta bora. Mafuta ya alizeti hutumiwa katika upishi, katika saladi, na kutengeneza siagi. Mbegu zake zina lishe bora kwani zina kati ya asilimia 18 na 22 za protini na aina nyingine za madini.
Watu wengi hupenda kula mbegu za alizeti zilizokaangwa na kutiwa chumvi. Mbegu za alizeti husagwa na unga wake huchanganywa na unga wa kuokea.
-