Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kichwa Kitukufu cha Biblia
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 9. Pasipo shaka ile mbegu ya Nyoka inatia ndani nini?

      9 Kwanza, kuna mbegu, au uzao, ya Nyoka. Hiyo ni nini? Hakika hii inatia ndani wale viumbe wengine wa roho waliojiunga na Shetani katika uasi wake na ambao hatimaye ‘walitupwa chini pamoja naye’ kwenye makao ya kidunia. (Ufunuo 12:9) Kwa kuwa Shetani, au Beelzebuli, ndiye “mtawala wa roho waovu,” ni wazi kwamba wao wanafanyiza tengenezo lake lisiloonekana.—Marko 3:22, NW; Waefeso 6:12.

      10. Biblia inatambulishaje wengine kuwa sehemu ya mbegu ya Shetani?

      10 Zaidi, Yesu aliwaambia viongozi wa kidini Wayahudi wa siku yake hivi: “Ninyi ni wa baba yenu, Ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzitenda.” (Yohana 8:44) Kwa kumpinga Yesu Mwana wa Mungu, hao viongozi wa kidini walionyesha kwamba wao pia walikuwa uzao wa Shetani. Walikuwa sehemu ya mbegu ya Shetani, wakitumikia yeye akiwa baba yao wa mfano. Wanadamu wengine wengi katika muda wote wa historia vivyo hivyo wamejitambulisha wenyewe kwa kufanya mapenzi ya Shetani, hasa katika kupinga na kunyanyasa wanafunzi wa Yesu. Kwa ujumla, wanadamu hawa wanaweza kuelezwa kuwa wakifanyiza tengenezo la Shetani lionekanalo duniani.—Ona Yohana 15:20; 16:33; 17:15.

  • Kichwa Kitukufu cha Biblia
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 15. (a) Eleza kule kusitawishwa kwa mbegu ya Shetani ya kibinadamu na ya kimalaika. (b) Ni nini lililopata mbegu ya Shetani wakati wa Gharika ya siku ya Noa?

      15 Mbegu ya kibinadamu ya Shetani ilianza kudhihirika mapema sana katika historia ya aina ya binadamu. Mathalani, alikuwako Kaini, binadamu wa kwanza kuzaliwa, ‘aliyekuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake’ Abeli. (1 Yohana 3:12) Baadaye, Enoki alisema juu ya Yehova akija “pamoja na mamiriadi yake watakatifu, ili atekeleze hukumu dhidi ya wote, na kuwatia hatiani wote wasioogopa Mungu kuhusu matendo yao ya kutokuogopa Mungu waliyofanya kwa njia isiyo ya kuogopa Mungu, na kuhusu mambo yote ya kushtusha ambayo watenda dhambi wasioogopa Mungu walisema dhidi yake.” (Yuda 14, 15, NW) Zaidi ya hilo, malaika waasi walijiunga na Shetani wakawa sehemu ya mbegu yake. Hao “waliacha mahali pa kukaa pao wenyewe panapofaa” katika mbingu ili wajivike miili yenye mnofu na kuoa binti za wanadamu. Walizaa uzao mchanganyiko wa mababe yenye nguvu zipitazo za kibinadamu. Ulimwengu huo ukajaa jeuri na ubaya, hivi kwamba Mungu aliuharibu katika Gharika, Noa mwaminifu na jamaa yake wakiwa ndio mnofu wa kibinadamu pekee uliookoka. Malaika wasiotii—sasa wakiwa roho waovu chini ya udhibiti wa Shetani—walilazimika kuacha wake na watoto wa mchanganyiko wao waliohukumiwa maangamizi. Walivua miili yenye mnofu, wakarudi kwenye milki ya kiroho ambako wanangojea kufikilizwa kwa hukumu inayokaribia kasi ya Mungu juu ya Shetani na mbegu yake.—Yuda 6, NW; Mwanzo 6:4-12; 7: 21-23; 2 Petro 2:4, 5.

      16. (a) Ni mtawala jeuri gani aliyetokea baada ya Gharika, na alionyeshaje alikuwa sehemu ya mbegu ya Shetani? (b) Mungu alizuiaje wale ambao wangekuwa wajenzi wa mnara wa Babuloni?

      16 Muda mfupi baada ya Gharika kuu, mtawala jeuri jina lake Nimrodi alitokea duniani. Biblia inamweleza kuwa “mwindaji mwenye nguvu katika kupingana na Yehova”—akiwa kweli kweli sehemu ya mbegu ya Nyoka. Kama vile Shetani, yeye alionyesha roho ya uasi akajenga jiji la Babeli, au Babuloni, kwa kukaidi kusudi la Yehova la kutaka aina ya binadamu isambae na kuijaza dunia. Kitovu cha Babuloni kilikuwa kiwe mnara mkubwa “ukiwa na kilele chao katika mbingu.” Mungu alizuia hawa ambao wangekuwa wajenzi wa mnara huo. Alichafua lugha yao “akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote” lakini akaruhusu Babuloni wenyewe ubaki.—Mwanzo 9:1; 10:8-12, NW; 11:1-9.

      Serikali Kubwa za Kisiasa Zatokea

      17. Kadiri aina ya binadamu ilivyoongezeka, ni sehemu gani ya jamii ya kibinadamu yenye ufisadi iliyotokea mbele, na likiwa tokeo, ni milki gani kubwa-kubwa zilizoinuka?

      17 Katika Babuloni zilitokea sehemu za jamii ya kibinadamu zilizositawi kwa kukaidi enzi kuu ya Yehova. Mojapo hizo ilikuwa ya kisiasa. Kadiri aina ya binadamu ilivyoongezeka, wanadamu wengine wenye kujitakia makuu walifuata kielelezo cha Nimrodi katika kunyakua mamlaka. Mwanadamu akaanza kutawala mwanadamu kwa umizo lake. (Mhubiri 8:9) Mathalani, katika siku za Abrahamu, Sodoma, Gomora, na majiji yaliyokuwa karibu yalikuja kuwa chini ya udhibiti wa wafalme kutoka Shinari na mabara mengine ya mbali. (Mwanzo 14:1-4) Hatimaye, makamambe wa kivita na kitengenezo waliunda milki kubwa-kubwa wajiletee wenyewe utajiri na utukufu. Biblia inarejezea baadhi ya hizi, kutia na Misri, Ashuru, Babuloni, Umedi-Ajemi, Ugiriki, na Roma.

      18. (a) Watu wa Mungu wanachukua mwelekeo gani kuhusu watawala wa kisiasa? (b) Mamlaka za kisiasa nyakati nyingine zimetumikiaje masilahi ya Mungu? (c) Watawala wengi wamejionyeshaje kuwa sehemu ya mbegu ya Nyoka?

      18 Yehova alivumilia kuwako kwa serikali hizi kubwa za kisiasa, na watu wake walizitolea utii wa kadiri walipoishi katika mabara yaliyo chini ya udhibiti wazo. (Warumi 13:1, 2) Nyakati nyingine, mamlaka za kisiasa hata zilitumikia mwendelezo wa makusudi ya Mungu au zikiwa himaya kwa watu wake. (Ezra 1:1-4; 7:12-26; Matendo 25:11, 12; Ufunuo 12:15, 16) Hata hivyo, watawala wengi wa kisiasa wamepinga kikatili ibada ya kweli, wakijionyesha wenyewe kuwa sehemu ya mbegu ya Nyoka.—1 Yohana 5:19.

      19. Serikali za ulimwengu zinatolewaje taswira katika kitabu cha Ufunuo?

      19 Kwa sehemu iliyo kubwa, utawala wa mwanadamu umeshindwa kwa kusikitisha kutuletea sisi binadamu furaha au kutatua matatizo yetu. Yehova ameruhusu aina ya binadamu ijaribie kila aina ya serikali, lakini yeye hakubali ufisadi au njia ambayo katika hiyo serikali zimetawala vibaya watu. (Mithali 22:22, 23) Ufunuo unatoa taswira ya serikali za ulimwengu zenye kuonea kuwa zikifanyiza hayawani-mwitu mkubwa mno na mwenye kiburi.—Ufunuo 13:1, 2.

      Wafanya Biashara Wenye Ubinafsi

      20, 21. Ni kikundi gani cha pili ambacho lazima kitiwe pamoja na “makamanda wa kivita” na “wanaume wakakamavu” kuwa ni mbegu mbovu ya Shetani, na kwa nini?

      20 Kwa kufungamana karibu-karibu na viongozi wa kisiasa, walitokea wanabiashara wasiofuata haki wa bidhaa zinazoonekana. Maandishi yaliyofukuliwa katika magofu ya Babuloni la kale yanaonyesha kwamba shughuli za kibiashara zenye kutumia hali mbaya za wanadamu wenzi kwa kujifaidi zilizoelewa sana huko nyuma. Wanabiashara wa ulimwengu wameendelea kujifaidi kwa ubinafsi kufika leo hii, hali katika mabara mengi wachache wamekuwa matajiri sana huku walio wengi wakinyong’onyea katika ufukara. Katika hiki kizazi cha kiviwanda, wanabiashara na watengeneza-bidhaa wamefanya pato kubwa kwa kuzipa serikali za kisiasa marundo mengi ya silaha haribifu za kivita na za kiibilisi, kutia na silaha za maangamizi makubwa ambazo sasa zinawahangaisha sana wanadamu. Watu mashuhuri wa kibiashara wenye pupa na hawa wengine wa aina yao lazima watiwe pamoja na “makamanda wa kivita” na “wanaume wakakamavu” kuwa ni wa mbegu mbovu ya Shetani. Wote hao ni sehemu ya tengenezo la kidunia ambalo Mungu na Kristo wanahukumu kuwa lastahili kufishwa.—Ufunuo 19:18, NW.

      21 Ni lazima sehemu ya tatu ya jamii ya kibinadamu ambayo inastahili hukumu kali ya Mungu iongezwe kwenye siasa zenye ufisadi na biashara yenye pupa. Ni nini hiyo? Huenda ukashangazwa na yanayosemwa na Ufunuo juu ya muundo huo wa tufe lote unaojulikana sana.

      Babuloni Mkubwa

      22. Ni dini ya aina gani iliyositawi katika Babuloni la kale?

      22 Kujengwa kwa Babuloni la kale hakukuwa shughuli ya kisiasa tu. Kwa kuwa jiji hilo lilisimamishwa kwa kukaidi enzi kuu ya Yehova, dini ilihusika. Kweli kweli, Babuloni la kale likaja kuwa chemchemi ya ibada ya sanamu ya kidini. Makuhani walo walifundisha mafundisho yenye kumvunjia Mungu heshima, kama vile kuokoka kwa nafsi ya kibinadamu baada ya kifo na kwamba baada ya hapo kuna mahali pa hofu ya milele na mateso yenye kusimamiwa na roho waovu. Walisitawisha ibada ya viumbe na umayamaya wa miungu ya kiume na ya kike. Walitunga hadithi za uwongo za kuelezea asili ya dunia na mwanadamu juu yayo na wakafanya sherehe na dhabihu zenye kushusha tabia, eti ili kuhakikisha uwezo wa kuzaa watoto na ukuzaji mazao, na ushindi katika vita.

      23. (a) Walipokuwa wakisambaa kutoka Babuloni, watu walienda na nini, kukiwa na tokeo gani? (b) Ufunuo unarejezea milki ya dini bandia yenye kuenea ulimwenguni pote kwa jina gani? (c) Ni dhidi ya nini dini bandia imepiga vita sikuzote?

      23 Vikundi mbalimbali vya lugha kutoka Babuloni viliposambaa juu ya dunia, vilienda na dini ya Kibabuloni. Kwa njia hiyo, sherehe na itikadi zinazofanana na zile za Babuloni la kale zikasitawi miongoni mwa wakazi wa awali wa Ulaya, Afrika, mabara ya Amerika, Mashariki ya Mbali, na Bahari za Kusini; na nyingi za itikadi hizi zinaendelea hadi leo hii. Basi, kwa kufaa, Ufunuo unarejezea milki ya dini bandia yenye kuenea ulimwenguni pote kuwa jiji lenye jina Babuloni Mkubwa. (Ufunuo, sura za 17, 18) Popote ilipopandwa, dini bandia imechipusha ukuhani mwingi wenye uonevu, ushirikina, utovu wa maarifa, na ukosefu wa adili. Imekuwa chombo chenye nguvu nyingi mkononi mwa Shetani. Sikuzote Babuloni Mkubwa amepiga vita vikali dhidi ya ibada ya kweli ya Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova.

      24. (a) Nyoka aliwezaje kuchubua Mbegu ya mwanamke ‘kisiginoni’? (b) Kwa nini kuchubuliwa kwa mbegu ya mwanamke kunasimuliwa kuwa jeraha tu la kisigino?

      24 Wakiwa sehemu yenye kulaumika zaidi sana ya mbegu ya Nyoka, waandishi na Mafarisayo katika dini ya Kiyahudi ya karne ya kwanza waliongoza katika kunyanyasa na mwishowe kuua kimakusudi mwakilishi wa kwanza wa mbegu ya mwanamke. Hivyo, Nyoka aliweza ‘kuchubua [“mbegu”] kisiginoni.’ (Mwanzo 3:15, NW; Yohana 8:39-44; Matendo 3:12, 15)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki