-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Ile Mbegu Yavumilia
17. (a) Fumbo la maneno la Yesu la ngano na magugu lilitabiri nini? (b) Ni jambo gani lililotukia katika 1918, likitokeza kukataliwa gani na kuwekwa rasmi gani?
17 Katika fumbo lake la maneno la ngano na magugu, Yesu alitabiri ule wakati wa giza ambao ungekuwako wakati Jumuiya ya Wakristo ilitawala ikiwa na mamlaka yote. Hata hivyo, kupitia karne zote za uasi-imani, kungekuwako Wakristo mmoja mmoja wa mfano wa ngano, wapakwa-mafuta halisi. (Mathayo 13:24-29, 36-43) Hivyo, wakati siku ya Bwana ilipopambazuka katika Oktoba 1914, Wakristo wa kweli walikuwa wangali wapo duniani. (Ufunuo 1:10) Inaonekana kwamba Yehova alikuja kwenye hekalu lake la kiroho kwa ajili ya kuhukumu karibu miaka mitatu na nusu baadaye, katika 1918, akiandamana na Yesu akiwa “mjumbe wa agano” wake. (Malaki 3:1; Mathayo 13:47-50) Ulikuwa wakati wa kukataa hatimaye wale Wakristo bandia na kuweka rasmi ‘yule mtumwa mwaminifu na mwenye akili juu ya mali yake yote.’—Mathayo 7:22, 23; 24:45-47.
18. Ni “saa” ipi iliyokuja katika 1914, nao ulikuwa wakati wa yule mtumwa kufanya nini?
18 Pia ulikuwa wakati wa mtumwa huyu kutoa uangalifu wa pekee kwa vile vitu vilivyoandikwa katika zile jumbe za Yesu zilizopelekwa kwa makundi saba, kama tunavyoona kutokana na mambo yaliyotaarifiwa humo. Mathalani, Yesu anarejeza kwenye kuja kwake kuhukumu makundi, hukumu ambayo ilianza katika 1918. (Ufunuo 2: 5, 16, 22, 23; 3:3) Yeye anasema juu ya kulipa himaya kundi la Filadelfia juu ya “ile saa ya mtihani ambayo yapasa ije juu ya dunia yote nzima inayokaliwa.” (Ufunuo 3:10, 11, NW) Hii “saa ya mtihani” inawasili inapopambazuka tu siku ya Bwana katika 1914, ambayo baada ya hiyo Wakristo walitahiniwa kwa habari ya ushikamanifu wao kwa Ufalme wa Mungu uliosimamishwa.—Linga Mathayo 24:3, 9-13.
19. (a) Yale makundi saba yanafananisha nini leo? (b) Ni nani ambao wameshirikiana na Wakristo wapakwa-mafuta wakiwa hesabu kubwa-kubwa na kwa nini lile shauri la Yesu na hali anazoeleza Yesu huhusu wao pia? (c) Imetupasa sisi tuzioneje zile jumbe za Yesu kwa yale makundi saba ya karne ya kwanza?
19 Kwa sababu hii, maneno ya Yesu kwa yale makundi yamekuwa na utumizi wayo mkubwa tangu 1914. Katika mazingira haya, yale makundi saba yanafananisha makundi yote ya Wakristo wapakwa-mafuta katika kipindi cha hii siku ya Bwana.
-
-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Mapema katika 1918 ule utendaji wa Ufalme wa watu wa Yehova ulikutana na upinzani mkubwa. Ulikuwa wakati wa kutahini duniani pote, na wale waoga walipepetwa wakatupwa nje. Katika Mei 1918 viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo walichochea kufungwa gerezani kwa maofisa wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi, lakini miezi tisa baadaye hao waliachiliwa. Baadaye, yale mashtaka ya bandia yaliyokuwa dhidi yao yaliondolewa. Tangu 1919 tengenezo la watu wa Mungu, likiwa limejaribiwa na kusafishwa, lilisonga mbele kwa bidii likatangaze Ufalme wa Yehova kwa njia ya Kristo Yesu kuwa ndilo tumaini pekee kwa aina ya binadamu.—Malaki 3:1-3.
-