-
“Kujijenga Wenyewe juu ya Imani Yenu Iliyo Takatifu Zaidi”“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
Mwanasarakasi huuzoeza mwili wake kwa kufanya mazoezi
12 Tulipozaliwa, miili yetu haikuwa imezoezwa. Kwa mfano, mtoto mchanga hatambui mahali mikono au miguu yake ilipo. Kwa hiyo, yeye hutupa-tupa mikono yake, na hata kujigonga-gonga kwenye uso, jambo ambalo linamuudhi na kumshangaza. Kadiri anavyotumia viungo vyake siku baada ya siku, ndivyo mwili wake unavyozoezwa. Mtoto huyo huanza kutambaa, kisha hutembea, na mwishowe hata anaweza kukimbia.a
-
-
“Kujijenga Wenyewe juu ya Imani Yenu Iliyo Takatifu Zaidi”“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
a Wanasayansi wanasema kwamba sisi husitawisha uwezo wa kutambua mahali mwili wetu ulipo na mahali miguu na mikono yetu ilipo. Kwa mfano, uwezo huo hukuwezesha kupiga makofi ukiwa umefunga macho. Mgonjwa mmoja aliyepoteza uwezo huo alishindwa kusimama, kutembea, au hata kuketi.
-