Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jerome—Mtangulizi Mwenye Kubishaniwa Katika Utafsiri wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Januari 1
    • Ili kutafsiri Maandiko ya Kiebrania, Jerome alinuia kuitumia Septuagint ikiwa msingi wa tafsiri yake. Wengi waliiona tafsiri hiyo ya Kigiriki ya Maandiko ya Kiebrania, ambayo ilitafsiriwa mara ya kwanza katika karne ya tatu K.W.K., kuwa ilipuliziwa moja kwa moja na Mungu. Kwa hiyo, Septuagint ilienezwa sana miongoni mwa Wakristo waliosema Kigiriki wakati huo.

      Hata hivyo, Jerome alipoendelea na kazi yake, alipata mambo yasiyopatana kati ya hati za Kigiriki, ambayo ni sawa na yale aliyopata katika hati za Kilatini. Jerome akavunjika moyo zaidi. Hatimaye, akakata kauli kwamba ili kutokeza tafsiri inayoweza kutumainiwa, lazima apuuze hati za Kigiriki, Septuagint ikiwa miongoni mwao, na aende moja kwa moja kwa maandishi-awali ya Kiebrania.

      Uamuzi huo ulisababisha upinzani mkali. Baadhi ya watu wakamwita Jerome mpotoshaji wa maandiko, mwenye kumkufuru Mungu na mwenye kuacha mapokeo ya kanisa kwa kupendelea Wayahudi. Hata Augustine—mwanatheolojia mkuu wa kanisa wakati huo—alimsihi sana Jerome ayarudie maandishi ya Septuagint, akisema: “Ikiwa tafsiri yako itaanza kusomwa na wote katika makanisa mengi, hilo litakuwa jambo la kuhuzunisha sana kwa sababu, wakati wa kusoma Andiko, lazima tofauti zitatokea baina ya Makanisa ya Kilatini na Makanisa ya Kigiriki.”

      Naam, hofu ya Augustine ilikuwa kwamba huenda kanisa lingegawanyika ikiwa makanisa ya Magharibi yangetumia maandishi ya Kilatini ya Jerome—yanayotegemea maandishi ya Kiebrania—huku makanisa ya Kigiriki ya Mashariki yakiwa yangali yanatumia tafsiri ya Septuagint.b Kwa kuongezea, Augustine alitoa maoni yenye mashaka juu ya kuiacha Septuagint kwa kupendelea tafsiri ambayo ni Jerome pekee angeweza kuitetea.

  • Jerome—Mtangulizi Mwenye Kubishaniwa Katika Utafsiri wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Januari 1
    • Septuagint yaendelea kutumiwa katika Jumuiya ya Wakristo ya Mashariki hadi leo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki