Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke Yake
    Amkeni!—2006 | Mei
    • Alijifunza kwamba Konstantino na waandamizi wake waliendeleza mafundisho bandia ambayo yaliongoza kwenye kukubaliwa kwa Utatu kuwa fundisho rasmi. Alipokuwa na umri wa miaka 20, Servetus alichapisha kitabu chake On the Errors of the Trinity, kitabu ambacho kilimfanya awe shabaha kuu ya Baraza la Kuhukumu Wazushi.

      Servetus aliona mambo kihalisi. Aliandika hivi: “Katika Biblia, hakuna mahali ambapo Utatu unatajwa. . . . Tunapata kumjua Mungu, si kupitia maoni ya hali ya juu ya kifalsafa, bali kupitia Kristo.”c Pia alifikia mkataa kwamba roho takatifu si mtu, bali, ni nguvu za Mungu zikitenda.

      Watu fulani walikubaliana na maoni ya Servetus. Sebastian Franck, Mprotestanti aliyeshiriki katika yale Marekebisho Makubwa ya Kidini, aliandika hivi: “Mhispania, Servetus, anabisha katika maandishi yake kwamba kuna Mungu mmoja tu. Kanisa la Roma linadai kwamba kuna watu watatu katika Mungu mmoja. Mimi ninakubaliana na Mhispania huyo.” Hata hivyo, Servetus hakusamehewa na Kanisa Katoliki la Roma na makanisa ya Waprotestanti kwa kupinga fundisho lao la msingi.

  • Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke Yake
    Amkeni!—2006 | Mei
    • c Katika kitabu chake A Statement Regarding Jesus Christ, Servetus alifafanua fundisho la Utatu kuwa lenye kutatanisha, na akasema kwamba “hakuna hata silabi moja” katika Maandiko inayotetea fundisho hilo.

  • Michael Servetus—Alitafuta Ukweli Akiwa Peke Yake
    Amkeni!—2006 | Mei
    • [Picha katika ukurasa wa 19]

      Ukurasa wa kwanza wa kitabu “On the Errors of the Trinity”

      [Hisani]

      From the book De Trinitatis Erroribus, by Michael Servetus, 1531

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki