-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na mimi nikaona hayawani-mwitu akipanda kutoka bahari, mwenye pembe kumi na vichwa saba, na juu ya pembe zake mataji kumi, lakini juu ya vichwa vyake majina yenye kufuru.
-
-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Vichwa saba vya huyu hayawani-mwitu husimama kwa ajili ya serikali sita kubwa za ulimwengu ambazo zimeelezwa katika historia ya Biblia kufikia siku ya Yohana—Misri, Ashuru, Babuloni, Umedi-Uajemi, Ugiriki, na Roma—na serikali kubwa ya ulimwengu ya saba iliyotolewa unabii kutokea baadaye.—Linga Ufunuo 17:9, 10.
6. (a) Vichwa saba vya hayawani-mwitu vilichukua uongozi katika nini? (b) Roma ilitumiwaje na Yehova katika kufikiliza hukumu zake mwenyewe juu ya mfumo wa mambo wa Kiyahudi, na Wakristo katika Yerusalemu walikuwa katika hali gani?
6 Ni kweli, kumekuwako serikali nyinginezo kubwa za ulimwengu katika historia mbali na zile saba—kama vile hayawani-mwitu ambaye Yohana aliona alivyokuwa na mwili pamoja na vichwa saba na pembe kumi. Lakini vichwa saba huwakilisha zile serikali kubwa ambazo, kila mojapo katika zamu yayo, imechukua uongozi katika kuonea watu wa Mungu. Katika 33 W.K., wakati Roma ilipokuwa mamlaka kuu yenye kutawala, Shetani alitumia hicho kichwa cha hayawani-mwitu kuua Mwana wa Mungu. Wakati huo, Mungu aliuacha mfumo wa mambo wa Kiyahudi usioaminika na baadaye, katika 70 W.K., akaruhusu Roma itekeleze hukumu yake juu ya taifa hilo. Kwa furaha, Israeli wa kweli wa Mungu, kundi lililopakwa mafuta la Wakristo, alikuwa ameonywa kimbele, na wale ambao walikuwa katika Yerusalemu na Yudea walikuwa wamekimbilia usalama ng’ambo ya Mto Yordani.—Wagalatia 6:16; Mathayo 24:15, 16.
7. (a) Kungetukia nini wakati umalizio wa mfumo wa mambo ungewasili na siku ya Bwana kuanza? (b) Ni nini kilichothibitika kuwa ndicho kichwa cha saba cha hayawani-mwitu wa Ufunuo 13:1, 2?
7 Hata hivyo, kufikia mwisho wa karne ya kwanza W.K., wengi katika hili kundi la mapema walikuwa wameanguka kutoka ukweli, na ngano ya kweli ya Kikristo, “wale wana wa ufalme,” ilikuwa imesongwa sana na magugu, “wale wana wa yule mwovu.” Lakini wakati umalizio wa mfumo wa mambo ulipowasili, Wakristo wapakwa-mafuta walitokea tena wakiwa kikundi kilichopangwa kitengenezo. Wakati wa siku ya Bwana, ulikuwa umefika wakati wa waadilifu ‘waangaze kwa uangavu kama jua.’ Kwa sababu hiyo, kundi la Kikristo lilipangwa kitengenezo kwa ajili ya kazi. (Mathayo 13:24-30, 36-43, NW) Kufikia wakati huo, Milki ya Roma haikuwapo tena. Milki kubwa ya Uingereza, pamoja na United States ya Amerika yenye nguvu nyingi, zilishikilia kitovu cha jukwaa la ulimwengu. Hii serikali ya ulimwengu ya uwili ilithibitika kuwa ndiyo kichwa cha saba cha hayawani-mwitu.
-
-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
10. (a) Ni nini inayoonyeshwa na uhakika wa kwamba juu ya kila mojapo pembe kumi palikuwa na taji? (b) Pembe kumi na mataji kumi huwakilisha nini?
10 Hayawani-mwitu ana pembe kumi juu ya vichwa vyake saba. Labda kila kimoja cha vichwa vinne kilikuwa na upembe mmoja na kila kimoja cha vichwa vitatu kilikuwa na pembe mbili. Zaidi ya hilo, alikuwa na mataji kumi juu ya pembe zake. Katika kitabu cha Danieli, hayawani wenye kuhofisha wanaelezwa, na hesabu ya pembe yapasa ifasiriwe kihalisi. Mathalani, pembe mbili za kondoo-dume huwakilisha milki ya ulimwengu yenye washirika wawili, Umedi na Uajemi, hali pembe nne zilizo juu ya mbuzi huwakilisha milki nne zilizokuwako wakati ule ule ambazo zilikua kutokana na milki ya Ugiriki ya Aleksanda Mkuu. (Danieli 8:3, 8, 20-22) Hata hivyo, juu ya hayawani ambaye Yohana aliona hesabu ya pembe kumi yaonekana kuwa ya ufananisho. (Linga Danieli 7:24; Ufunuo 17:12.) Zinawakilisha ukamili wa serikali zenye enzi ambazo hujumlika kuwa tengenezo la kisiasa la Shetani. Pembe hizi zote ni zenye jeuri na zenye kutaka vita, lakini kama inavyoonyeshwa na vichwa saba, ukichwa hukaa katika serikali kubwa moja ya ulimwengu, wakati mmoja. Hali kadhalika, yale mataji kumi huonyesha kwamba serikali zote zenye enzi zingetumia mamlaka yenye kutawala wakati ule ule mmoja na dola kuu au serikali kubwa ya ulimwengu, ya wakati huo.
11. Ni nini kinachoonyeshwa na uhakika wa kwamba hayawani-mwitu ana “juu ya vichwa vyake majina ya kufuru”?
11 Huyo hayawani-mwitu ana “juu ya vichwa vyake majina yenye kufuru,” akijifanyia madai yanayoonyesha utovu mkubwa wa kustahi Yehova Mungu na Kristo Yesu. Ametumia majina ya Mungu na Kristo kuwa kisingizio cha kutimizia makusudi yake ya kisiasa; naye amecheza pamoja na dini bandia, hata kukubali viongozi wa kidini washiriki sehemu katika mambo ya siasa. Mathalani, Nyumba ya Mabwana ya Uingereza hutia ndani maaskofu. Makardinali wa Kikatoliki wamekuwa na vyeo vya umashuhuri katika Ufaransa na Italia, na hivi majuzi mapadri wametwaa vyeo vya kisiasa katika Amerika ya Kilatini. Serikali huchapa shime za kidini, kama “IN GOD WE TRUST” (Sisi Twaitibari Mungu), kwenye noti zao za benki, na juu ya sarafu zao zinadai kwamba watawala wazo wana kibali cha kimungu, wakitaarifu, mathalani, kwamba hao wanawekwa rasmi “kwa neema ya Mungu.” Kwa kweli yote haya ni makufuru, kwa kuwa hujaribu kumhusisha Mungu katika uwanja wa kisiasa wa kitaifa wenye kutiwa uchafu.
-
-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
13. (a) Ni baa gani linalompata hayawani-mwitu mapema katika siku ya Bwana? (b) Ni jinsi gani hayawani-mwitu mzima wote aliumia wakati kichwa kimoja kilipopokea dharuba-kifo?
13 Mapema katika siku ya Bwana, baa linampiga hayawani-mwitu. Yohana huripoti: “Na mimi nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimechinjwa hadi kifo, lakini dharuba-kifo yake ikaponeshwa, na dunia nzima yote ikafuata hayawani-mwitu kwa kusifu mno.” (Ufunuo 13:3, NW) Mstari huu husema kwamba kichwa kimoja cha huyu hayawani-mwitu kilipokea dharuba ya kifo, lakini mstari wa 12 husema kana kwamba hayawani mzima wote aliumia. Ni kwa nini hivyo? Basi, si vichwa vyote vya huyo hayawani vinavyodhibiti pamoja mamlaka kuu. Kila kimoja katika zamu yacho kimepiga ubwana juu ya aina ya binadamu, hasa juu ya watu wa Mungu. (Ufunuo 17:10) Hivyo, siku ya Bwana inapoanza, kuna kichwa kimoja tu, kile cha saba, kikitenda kuwa ndicho serikali kubwa ya ulimwengu yenye kutawala. Dharuba ya kifo kwenye kichwa hicho humletea hayawani-mwitu mzima wote taabu kubwa.
14. Ni lini dharuba-kifo ilipopigwa, na ofisa mmoja wa kijeshi alielezaje tokeo layo juu ya hayawani-mwitu wa Shetani?
14 Ni nini iliyokuwa dharuba-kifo? Baadaye, huitwa dharuba-upanga, na upanga ni ufananisho wa vita. Dharuba-kifo hii, iliyopigwa mapema katika siku ya Bwana, lazima ihusiane na vita ya ulimwengu ya kwanza, iliyokumba na ikamkausha hayawani-mwitu wa kisiasa wa Shetani. (Ufunuo 6:4, 8;13:14) Mtunga vitabu Maurice Genevoix, aliyekuwa ofisa wa kijeshi katika vita hiyo, alisema kuihusu hivi: “Kila mmoja anakubali katika kutambua kwamba katika historia ya aina ya binadamu kwa ujumla, tarehe chache zimekuwa na umaana wa Agosti 2, 1914. Kwanza Ulaya na upesi baadaye karibu binadamu wote walijikuta wametumbukia ndani ya tukio lenye kuhofisha. Kawaida, miafaka, sheria za kiadili, misingi yote ilitikisika; kutoka siku moja hadi inayofuata, kila kitu kilitiliwa shaka. Tukio hilo lilipasa kuzidi mabashiri ya kisilika na mataraja ya kiasi pia. Likiwa kubwa mno, lenye machafuko, lenye kutia hofu, lingali laburuta sisi katika njia yalo.”—Maurice Genevoix, mshiriki wa Acadeʹmie Française, aliyenukuliwa katika kitabu Promise of Greatness (1968).
15. Ni jinsi gani kichwa cha saba cha hayawani mwitu kilipokea dharuba-kifo?
15 Vita hiyo ilikuwa msiba mkubwa wa kichwa kikuu cha saba cha hayawani-mwitu. Pamoja na mataifa mengine ya Ulaya, Uingereza ilipoteza vijana wayo kwa hesabu yenye kuumiza sana. Katika pigano moja pekee, lile Pigano la Mto Somme katika 1916, kulikuwa na askari-jeshi 420,000 wa Uingereza waliokufa au kupotea vitani, pamoja na 194,000 wa Ufaransa na 440,000 wa Ujeremani—jumla ya watu zaidi ya 1,000,000 waliokufa au kupotea vitani! Kiuchumi, vilevile, Uingereza—pamoja na sehemu nyingine ya Ulaya—ilivunjwavunjwa. Milki kubwa mno ya Uingereza ilitetereka chini ya hilo pigo na haikupona kikamili kamwe. Kweli kweli, vita hiyo, ikiwa na mataifa mashuhuri 28 ilifanya ulimwengu mzima wote uyumbeyumbe kana kwamba kwa pigo la kifo. Katika Agosti 4, 1979, miaka 65 tu baada ya kufyatuka Vita ya Ulimwengu 1, The Economist, la London, Uingereza lilieleza: “Katika 1914 ulimwengu ulipoteza ushikamano ambao haujaweza kuupata tena tangu hapo.”
16. Wakati wa vita ya ulimwengu ya kwanza, United States ilionyeshaje kwamba ilikuwa sehemu ya serikali kubwa ya ulimwengu ya uwili?
16 Wakati ule ule, ile Vita Kubwa, kama ilivyoitwa wakati huo, ilifungulia njia United States kuibuka waziwazi ikiwa sehemu ya Serikali Kubwa ya Ulimwengu ya Uingereza-Amerika. Katika miaka ya kwanza ya vita hiyo, maoni ya umma yaliondoa United States katika pambano hilo. Lakini kama alivyoandika mwanahistoria Esmé Wingfield-Stratford, hayo “yote yalikuwa swali la kama, katika saa hii ya hatari kubwa mno, Uingereza na United States zingezamisha tofauti zao katika kupata umoja [wao] wenye ushindi na udhamini wa pamoja.” Kama vile matukio yalivyopata kuwa, zilifanya hivyo. Katika 1917 United States ilichanga rasilimali na askari-jeshi ili kusaidia jitihada za Mataifa-Mafungamani yaliyokuwa yakiyumbayumba. Hivyo, kichwa cha saba, kikiunganisha Uingereza na United States, kikatokea kikiwa upande wenye kushinda.
17. Kukawa nini kwa mfumo wa kidunia wa Shetani baada ya vita?
17 Ulimwengu baada ya vita hiyo ulikuwa tofauti sana. Mfumo wa kidunia wa Shetani, ujapokuwa ulikumbwa na pigo la kifo, ulipona na ukawa wenye nguvu zaidi kuliko wakati wowote na hivyo ukasifiwa sana na wanadamu kwa sababu ya nguvu zao za kupona.
18. Inaweza kusemwaje kwamba aina ya binadamu kwa ujumla ‘imefuata hayawani-mwitu kwa kusifu mno’?
18 Mwanahistoria Charles L. Mee, Jr., anaandika: “Anguko la utaratibu wa kale [lililosababishwa na vita ya ulimwengu ya kwanza] lilikuwa utangulizi uliohitajiwa kabisa kwa mtandazo wa kujitawala, ule ukombozi wa mataifa mapya na matabaka, kuachiliwa kwa uhuru na kujitegemea kupya.” Chenye kuongoza katika mwendeleo wa kipindi hiki cha baada ya vita kilikuwa kichwa cha saba cha hayawani-mwitu, kikiwa sasa kimepona, na United States ya Amerika ikichukua daraka kuu. Hiyo serikali kubwa ya ulimwengu ya uwili ilichukua uongozi katika kutetea Ushirika wa Mataifa na Umoja wa Mataifa. Kufikia mwaka wa 2005, nguvu za kisiasa za U.S. zilikuwa zimeongoza mataifa yenye mapendeleo zaidi katika kubuni kiwango cha juu zaidi cha maisha, katika kupigana na magonjwa, na katika kuendeleza tekinolojia. Hata ilikuwa imepeleka watu 12 kwenye mwezi.
-