Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Neno la Mungu Hudumu Milele
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 1
    • (2) Mtu aliyekuwa wa kwanza kutafsiri kitabu cha Danieli kwa ajili ya Septuagint ya Kigiriki alijiamulia kutafsiri apendavyo. Aliongeza taarifa alizofikiri zingeeleza au kuboresha yaliyokuwamo katika maandishi ya Kiebrania. Aliondoa mambo madogo-madogo ambayo alifikiri yangekataliwa na wasomaji. Alipotafsiri unabii kuhusu wakati wa kutokea kwa Mesiya, upatikanao kwenye Danieli 9:24-27, alipotosha kipindi cha wakati kilichotaarifiwa na kuongeza, kubadili, na kubadilisha maneno, yaonekana akinuia kuufanya unabii uonekane kutegemeza shindano la Wamakabayo.

  • Neno la Mungu Hudumu Milele
    Mnara wa Mlinzi—1997 | Oktoba 1
    • Kupotoshwa kwa maneno katika Septuagint hakukumzuia Mesiya asije wakati uliotabiriwa kupitia nabii Danieli. Zaidi ya hilo, hata ingawa Septuagint ilikuwa ikitumika karne ya kwanza, kwa wazi Wayahudi walizoea kusikia Maandiko yakisomwa katika Kiebrania katika masinagogi yao. Tokeo ni kwamba, “watu walikuwa wakitarajia” wakati wa kutimizwa kwa unabii ulipokaribia. (Luka 3:15)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki