Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nabii Aliye Uhamishoni Apata Maono ya Wakati Ujao
    Biblia—Ina Ujumbe Gani?
    • Danieli apata kujua Masihi atafika wakati gani. Danieli aliambiwa wakati ambapo watu wa Mungu wangeweza kutazamia “Masihi Kiongozi” afike—Majuma 69 ya miaka baada ya amri ya kujengwa upya kuta za Yerusalemu kutolewa. Juma la kawaida lina siku saba; juma la miaka ni miaka saba. Amri hiyo ilitolewa muda mrefu baada ya wakati wa Danieli, yaani, mwaka wa 455 K.W.K. “Majuma” hayo 69 yalianza wakati huo na kuendelea kwa muda wa miaka 483, hadi mwaka wa 29 W.K. Katika sehemu inayofuata ya broshua hii, tutaona kilichotokea mwaka huo. Danieli aliona kimbele kwamba Masihi “angekatiliwa mbali,” au kuuawa, ili kufanya upatanisho wa dhambi.—Danieli 9:24-26.

  • Masihi Afika
    Biblia—Ina Ujumbe Gani?
    • Yohana alipombatiza Yesu, Yehova mwenyewe alisema kutoka mbinguni. Akitumia roho takatifu, alimweka rasmi Yesu kuwa Masihi na kusema: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa, ambaye nimemkubali.” (Mathayo 3:16, 17) Masihi aliyeahidiwa akawa amefika!

      Hilo lililotokea wakati gani? Mwaka wa 29 W.K., wakati ambapo ile miaka 483 iliyotabiriwa na Danieli ilipokamilika.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki