Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kunyanyasa Watoto Kingono—Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—1997 | Aprili 8
    • The Children’s Ombudsman, shirika la Sweden, liliwaambia wajumbe hivi: “Wakati ambapo uchunguzi umefanywa juu ya kile kisababishacho ukahaba wa watoto, hakuna shaka kwamba utalii [wa ngono] ndio mmojawapo visababishi vikuu.” Ripoti moja ilisema: “Kuongezeka kunakotazamisha kwa ukahaba wa watoto kwa miaka kumi iliyopita kunasababishwa moja kwa moja na biashara ya utalii. Ukahaba wa watoto ndio kivutio cha watalii kilicho kipya zaidi kinachoandaliwa na nchi zinazoendelea.” “Watalii wa ngono” kutoka, Ulaya, Marekani, Japani, na kwingineko hufanyiza uhitaji mkubwa wa makahaba watoto ulimwenguni pote. Shirika moja la ndege la Ulaya lilitumia mchoro wa katuni ulio wazi wa mtoto akiwa katika kikao cha kingono ili kuendeleza utalii wa ngono. Mashirika ya kupanga safari hupanga utalii wa ngono kwa maelfu kila mwaka.

  • Kunyanyasa Watoto Kingono—Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—1997 | Aprili 8
    • Kikundi chenye kushughulikia utalii wa kingono kilipendekeza kwamba pambano lifanywe kupitia elimu katika utaratibu wa masomo shuleni. Kwa kuongezea, habari dhidi ya unyanyasaji wa kingono wa watoto zapaswa kufikia wasafiri kotekote safarini—kabla ya kuondoka, wakati wa safari, na mwishoni mwa safari.

  • Kunyanyasa Watoto Kingono—Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—1997 | Aprili 8
    • Utalii wa Ngono—Kwa Nini Upo?

      (Baadhi ya sababu zinazofanya watalii wajihusishe katika ngono na watoto)

      (1) Kwa kuwa mtalii hajulikani na wenyeji anahisi akiwa amewekwa huru na vizuizi vya kijamii vya kwao

      (2) Kwa sababu ya kutofahamu sana au kutofahamu kabisa lugha ya wenyeji, watalii waweza kuongozwa vibaya kwa urahisi kufikiri kwamba kulipa ili kufanya ngono na watoto hukubalika kwa kawaida au ni njia ya kuwasaidia watoto kutoka kwenye umaskini

      (3) Mitazamo ya ubaguzi wa kijamii hufanya wageni wanyanyase wale ambao huwaona kuwa wa hali ya chini

      (4) Watalii hujihisi wakiwa matajiri wanapoona kwamba huduma za kingono ni za bei rahisi katika nchi zinazoendelea

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki