Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wamjua Shafani na Familia Yake?
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Desemba 15
    • Biblia humtaja “Shafani, mwana wa Azalia, mwana wa Meshulamu” kwa mara ya kwanza Yosia aliporudisha ibada ya kweli yapata mwaka wa 642 K.W.K. (2 Wafalme 22:3)

  • Je, Wamjua Shafani na Familia Yake?
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Desemba 15
    • Shafani Ategemeza Ibada ya Kweli

      Mnamo mwaka wa 642 K.W.K., Mfalme Yosia alipokuwa na umri wa miaka 25 hivi, tunaona Shafani anatumikia akiwa mwandishi na mnakili wa mfalme. (Yeremia 36:10) Kazi hiyo ilihusisha nini? Kichapo cha kitaalamu kilichotajwa juu kinasema kwamba mnakili na mwandishi wa mfalme alikuwa mshauri wake wa karibu, alisimamia mambo ya kifedha, alikuwa balozi stadi, alishughulika na masuala ya nchi za kigeni, alifahamu sheria za kimataifa, na mapatano ya biashara. Kwa hiyo, akiwa mwandishi wa mfalme, Shafani alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri zaidi katika ufalme huo.

      Miaka kumi kabla ya hapo, Yosia mchanga alikuwa ‘ameanza kumtafuta Mungu wa Daudi babaye.’ Yaonekana Shafani alikuwa na umri mkubwa kuliko Yosia na hivyo angeweza kuwa mshauri mzuri wa kiroho na pia angemwunga mkono Yosia katika kampeni yake ya kwanza ya kurudisha ibada ya kweli.a—2 Mambo ya Nyakati 34:1-8.

      Kazi ya kurekebisha hekalu ilipokuwa ikiendelea, “kitabu cha torati” kilipatikana, naye Shafani ‘akaanza kukisoma mbele ya mfalme.’ Yosia alishtushwa na mambo aliyosikia na hivyo akatuma wajumbe waliotumainika kwenda kwa Hulda nabii wa kike ili kupata habari kutoka kwa Yehova kuhusu kitabu hicho. Mfalme alionyesha kwamba anamtumaini Shafani na mwana wake Ahikamu kwa kuwaweka wawe miongoni mwa wajumbe hao.—2 Wafalme 22:8-14; 2 Mambo ya Nyakati 34:14-22.

      Hili ndilo Andiko pekee linaloonyesha jambo alilofanya Shafani. Katika mistari mingine ya Biblia, anatajwa tu kuwa baba au babu.

  • Je, Wamjua Shafani na Familia Yake?
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Desemba 15
    • a Shafani alikuwa na umri mkubwa kuliko Yosia, kwa sababu Ahikamu mwana wa Shafani alikuwa mtu mzima wakati Yosia alipokuwa na umri wa miaka 25 hivi.—2 Wafalme 22:1-3, 11-14.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki