-
Yehova Ni Mchungaji WetuMnara wa Mlinzi—2005 | Novemba 1
-
-
6. Kulingana na kamusi moja ya Biblia, mchungaji wa kale alifanya nini siku nzima?
6 Mchungaji wa kale alifanya nini siku nzima? Kamusi moja ya Biblia inaeleza hivi: “Mapema asubuhi aliwatoa kondoo zizini, kisha akawaongoza hadi malishoni huku akitembea mbele yao. Akiwa huko, aliwachunga siku nzima huku akihakikisha kwamba hakuna kondoo yeyote anayetanga-tanga, na iwapo mmoja wao angeponyoka na kuwaacha wengine bila yeye kujua, angemtafuta kwa bidii mpaka ampate na kumrudisha. . . . Usiku, alirudisha kundi zizini, akiwahesabu huku wakipita mlangoni chini ya fimbo ili kuhakikisha kwamba hakuna aliyekosekana. . . . Mara nyingi alilazimika kulinda zizi usiku ili kondoo wasishambuliwe na wanyama wa mwitu au wezi.”a
7. Kwa nini wakati mwingine mchungaji alihitaji kuwa mwenye subira na mwenye huruma zaidi?
7 Wakati mwingine kondoo wenye mimba na wale wachanga walihitaji subira na huruma zaidi. (Mwanzo 33:13) Kitabu kimoja kinachozungumzia Biblia kinasema hivi: “Mara nyingi kondoo huzaliwa mbali sana milimani. Mchungaji humlinda kwa makini mama aliye dhaifu kisha humbeba mwana-kondoo na kumpeleka zizini. Kwa siku kadhaa baada ya kuzaliwa, mpaka atakapoweza kutembea, huenda akambeba mikononi mwake au katika mapindo ya vazi lake la juu.” (Isaya 40:10, 11) Bila shaka, mchungaji mzuri alihitaji kuwa mwenye nguvu na mwenye huruma.
-