Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Viatu Vyako Vinakutoshea Vizuri?
    Amkeni!—2003 | Machi 8
    • Miguu Yako Hupimwaje?

      Kwa miaka mingi, Eric alikuwa akinunua viatu vya saizi 10 na nusu au saizi 11 vyenye upana wa wastani. Wakati huo, alikuwa akiumia kwa sababu kidole kimoja cha mguu wake kilikuwa kimejikunja na kuota sugu na vilevile kidole kikubwa cha mguu wake wa kushoto kilikuwa na kucha iliyoota kuelekea ndani. Daktari mmoja wa miguu alidokeza kwamba ingefaa aende kupimwa saizi ya miguu yake na mtu aliye na ujuzi huo. Eric alishangaa alipogundua kwamba ili viatu vimtoshee vizuri anapaswa kuvaa viatu vya saizi 12 na nusu vyenye upana wa A! Herufi “A” inaonyesha kwamba mtu ana mguu mwembamba.a Lakini, je, inatosha kujua tu urefu na upana wa viatu unavyostahili kuvaa? Ni njia ipi iliyo bora ya kupima miguu?

      Katika nchi fulani, kifaa kinachoitwa Brannock ndicho hutumiwa hasa kupimia miguu. (Ona picha.) Kifaa hicho kinaweza kutumiwa kuonyesha vipimo vitatu muhimu: urefu wa mguu wote, urefu unaoanzia kwenye kisigino hadi kwenye mfupa wa mviringo ulio chini ya kidole kikubwa, na upana unaopimwa kuanzia kwenye mfupa huo hadi kwenye kidole kidogo. Lakini, umbo na ukubwa wa kila mguu hutofautiana. Ndiyo sababu sisi hupima viatu kabla ya kuvinunua. Hata hivyo, kuna hatari fulani. Je, umewahi kupima viatu vilivyokuvutia sana kisha ukagundua kwamba vinakufinya kidogo? Labda vinakufinya kidogo tu au ni vikubwa kidogo. Na duka hilo halina viatu vingine vinavyokutoshea. Kisha muuzaji anakuambia: “Ah! Viatu hivi vitapanuka.” Unavinunua, halafu baada ya kuvitumia kwa siku chache au majuma kadhaa unaanza kujuta. Vidole vinaanza kuota sugu, kucha ya kidole kimoja inaanza kuota kuelekea ndani, au unapata uvimbe kwenye kidole kikubwa!

  • Je, Viatu Vyako Vinakutoshea Vizuri?
    Amkeni!—2003 | Machi 8
    • “Kusudi la kupima mguu si kumwezesha mtu ajue saizi ambayo itamtoshea, kama vile watu wengine wanavyodhania.” Kwa nini? Kwa sababu saizi ya viatu inategemea mambo mengi kama vile, urefu wa kisigino, mtindo, muundo, vifaa vilivyotumiwa, na kampuni iliyotengeneza viatu hivyo. Jambo hilo ni kweli kwani nchi nyingi sana zinatengeneza viatu kwa kutumia viwango tofauti-tofauti.

      Urefu wa mguu wako unapopimwa, vuta soksi mbele ili vidole vyako visijikunje, kwani hilo litafanya vipimo visiwe sahihi.

      Unapaswa kupimwa ukiwa umeketi au ukiwa umesimama? “Haifai kumpima mteja akiwa ameketi.” Kufanya hivyo kunatokeza vipimo visivyo sahihi. Basi, simama miguu yako inapopimwa. Naam, si mguu mmoja bali miguu yote miwili. Usifikiri kwamba mguu wako wa kushoto ndio mkubwa zaidi. Unapaswa kupimwa miguu yote miwili!

  • Je, Viatu Vyako Vinakutoshea Vizuri?
    Amkeni!—2003 | Machi 8
    • [Picha katika ukurasa wa 20]

      Kifaa cha Brannock

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki