Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ndugu Skiba anaendelea kusema: “Wakati mmoja ili niweze kufika Yekaterinburg kutoka Noril’sk, iliyoko kaskazini ya Mzingo wa Aktiki, nilihitaji kusafiri kwa ndege mbili, kwanza kutoka Noril’sk hadi Novosibirsk, kisha hadi Yekaterinburg. Safari hiyo ilionekana kana kwamba haitakwisha. Ndege tuliyotumia kutoka Noril’sk ilicheleweshwa kwa saa 12 hivyo mimi na mke wangu Lyudmila tulikaa siku nzima kwenye kituo cha ndege. Uzuri ni kwamba tulikuwa tumejifunza kufanya funzo letu la kibinafsi tunaposafiri.

  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mnamo 1996, huko Yekaterinburg, akina ndugu walichagua uwanja unaofaa wa michezo ili kufanyia kusanyiko la wilaya. Roman Skiba anakumbuka: “Nyasi ziliota kwenye mabenchi, na ndani ya uwanja mibetula ilikuwa na kimo cha mita mbili. Majuma matatu yalisalia kabla ya kusanyiko, na kulikuwa na makutaniko matatu katika jiji na vitongoji. Msimamizi wa uwanja alishirikiana nasi hata ingawa hakuelewa jinsi tunavyoweza kufanya kusanyiko katika uwanja huo. Akina ndugu walianza kazi, na siku iliyowekwa, uwanja ulikuwa unapendeza. Msimamizi hakuamini macho yake!” Akichochewa na uthamini, msimamizi aliruhusu Shule ya Utumishi wa Painia ifanywe kwenye jengo moja la uwanja huo. Ndugu mmoja anakumbuka, “Baada ya kusanyiko, uwanja huo ulianza tena kutumiwa kwa ajili ya michezo, nayo ilililetea jiji hilo mapato.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki