-
Sayari Ndogo, Nyotamkia, na Dunia—Je, Ziko Katika Mwendo wa Kugongana?Amkeni!—1999 | Januari 22
-
-
‘Mapema asubuhi mnamo Juni 30, kitu kisicho cha kawaida kilionekana katika kijiji fulani huko Siberia. Juu angani, wakulima waliona kitu kilichong’aa kwa uangavu mwingi; kilikuwa na uangavu mwingi sana usioweza kutazamwa kwa macho. Chini kwenye anga, upande uleule kulipokuwa na kitu hiki chenye kung’aa, wingu dogo jeusi lilionekana. Kitu hicho kiangavu kilipokaribia kufika ardhini, kilionekana kuwa kimesagwa kuwa mavumbi. Mahali kilipoanguka, kulitokea wingu kubwa la moshi mweusi, na mlipuko mkubwa ulisikika, kana kwamba ulitokana na lundo kubwa la majabali. Majengo yalitikisika, na ndimi za miale zilizogawanyika zilijitokeza juu ya wingu hilo. Wanakijiji walikimbia barabarani wakiwa na hofu. Wanawake wazee walilia; kila mtu alifikiri mwisho wa ulimwengu umewadia.’—Muhtasari wa ripoti iliyochapishwa katika gazeti la habari la Sibir, Irkutsk, Urusi, mnamo Julai 2, 1908.
WANAKIJIJI hao hawakutambua hata kidogo kwamba kitu fulani kutoka mbinguni kilikuwa kimelipuka tu juu ya vichwa vyao.
-
-
Sayari Ndogo, Nyotamkia, na Dunia—Je, Ziko Katika Mwendo wa Kugongana?Amkeni!—1999 | Januari 22
-
-
Mnamo Juni 30, 1908, sayari ndogo au kipande kikubwa cha nyotamkia kinachokadiriwa kuwa na upana unaopungua meta 100 kiliingia kwa mngurumo kwenye angahewa na kulipuka kilometa zipatazo kumi juu ya eneo lisilokuwa na watu wengi la Tunguska la Siberia, kama ilivyotajwa katika utangulizi. Mlipuko huo, uliokadiriwa kuwa wa megatoni 15, uliharibu eneo lenye kilometa mraba 2,000, ukiangusha miti, kuwasha mioto, na kuua kulungu. Ni watu wangapi ambao wangekufa iwapo mahali palipotokea mlipuko huo palikuwa eneo lenye watu wengi sana?
-