-
Mahali pa Muziki Katika Ibada ya KisasaMnara wa Mlinzi—1997 | Februari 1
-
-
Huenda wengine wakadai, ‘Siwezi kuimba wimbo vizuri’ au ‘nina sauti mbaya; hualika niimbapo sauti za juu.’ Hivyo, wao huona haya waimbapo, hata kwenye Jumba la Ufalme. Kweli ni kwamba hakuna sauti inayoinuliwa katika kumsifu Yehova iliyo “mbaya” kwa maoni yake. Sawa na vile sauti ya mtu ya kuongea iwezavyo kuboreshwa kwa mazoezi na kwa kufuata madokezo yenye kusaidia yanayotolewa katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi, ndivyo kuimba kwa mtu kuwezavyo kuboreshwa. Watu fulani wameboresha sauti zao kwa kuvuma tu wimbo wafanyapo kazi za kila siku. Kuvuma wimbo kwasaidia kulainisha sauti. Na kwa nyakati zifaazo tunapokuwa peke yetu au tunapofanya kazi mahali ambapo tusingesumbua wengine, kuimba melodia za Ufalme ni mazoezi mazuri kwa sauti na ni njia ya kumtia mtu katika hali ya akilini yenye shangwe, na ya pumziko.
Twaweza pia kutia moyo kuimbwa kwa nyimbo chache za Ufalme kwenye vikusanyiko. Kuimba huko, kunakofuatanishwa na ala kama vile gitaa au piano au na mirekodi ya piano ya Sosaiti, huandalia vikusanyiko vyetu mazingira ya kiroho. Kuimba huandaa pia msaada wa kujifunza nyimbo na kuziimba vizuri kwenye mikutano ya kutaniko.
-
-
Mahali pa Muziki Katika Ibada ya KisasaMnara wa Mlinzi—1997 | Februari 1
-
-
MADOKEZO KADHAA YA KUIMBA VIZURI ZAIDI
1. Shika kitabu cha wimbo kikiwa juu uimbapo. Hilo lamsaidia mtu apumue kikawaida zaidi.
2. Pumua kwa uzito mwanzoni mwa kila fungu la maneno.
3. Kukifungua kinywa wazi zaidi kuliko kawaida mwanzoni kutaongeza kiasili kiasi cha sauti na mlio wa sauti.
4. Zaidi ya yote, kazia fikira hisia ya wimbo unaoimbwa.
-