-
Usimpe Ibilisi NafasiMnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
-
-
Usimwige Mchongezi Mkuu
4. “Yule mwovu” alimchongeaje Mungu?
4 “Yule mwovu” anastahili kuitwa Ibilisi kwa kuwa yeye ni mchongezi. Uchongezi ni kusema uwongo kumhusu mtu mwingine ili kumdhuru au kumharibia jina. Mungu alimwagiza Adamu hivi: “Kuhusu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula, utakufa hakika.” (Mwanzo 2:17) Hawa alikuwa amejulishwa kuhusu agizo hilo, lakini Ibilisi alimwambia hivi kupitia nyoka: “Hakika hamtakufa. Kwa maana Mungu anajua kwamba siku ileile mtakapokula matunda yake macho yenu yatafunguliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” (Mwanzo 3:4, 5) Huo ulikuwa uchongezi mbaya dhidi ya Yehova Mungu!
-
-
Usimpe Ibilisi NafasiMnara wa Mlinzi—2006 | Januari 15
-
-
Biblia inamtaja Shetani kuwa “mshtaki wa ndugu zetu . . . , anayewashtaki mchana na usiku mbele za Mungu wetu.” (Ufunuo 12:10) Ndugu hao wanaoshtakiwa kwa uwongo ni Wakristo watiwa-mafuta ambao wako duniani katika siku hizi za mwisho.
-