-
Jitihada za Muda Mrefu za Kuboresha AfyaAmkeni!—2004 | Mei 22
-
-
Ndui Yashambulia Mabara ya Amerika
Columbus alipowasili West Indies mwaka wa 1492, alisema kwamba wenyeji walikuwa na ‘sura nzuri, maumbo mazuri, kimo cha wastani, na maungo.’ Hata hivyo, licha ya kuwa na afya nzuri, bado walikumbwa kwa urahisi na magonjwa yaliyoenea kutoka Ulaya.
Mnamo mwaka wa 1518, ugonjwa wa ndui ulizuka katika kisiwa cha Hispaniola. Waamerika wenyeji hawakuwa wameugua ugonjwa huo hapo awali, na matokeo yakawa mabaya sana. Mhispania mmoja aliyejionea hali hiyo, alikadiria kwamba watu elfu moja tu ndio waliookoka katika kisiwa hicho. Punde baadaye ugonjwa huo ulifika Mexico na Peru ukiwa na matokeo hayohayo.
Wakoloni Waingereza walipowasili Massachusetts huko Amerika Kaskazini katika karne iliyofuata, waligundua kwamba wakaaji wengi walikuwa wamekufa kutokana na ndui. Kiongozi wao, John Winthrop, aliandika hivi: “Karibu wenyeji wote wamefagiliwa mbali na ugonjwa wa ndui.”
-
-
Jitihada za Muda Mrefu za Kuboresha AfyaAmkeni!—2004 | Mei 22
-
-
Bila shaka si wenyeji wa Amerika tu walioathiriwa na ndui. Kitabu Scourge—The Once and Future Threat of Smallpox kinasema hivi: “Katika historia yote ya binadamu, ndui iliua mamia ya mamilioni ya watu, wengi kuliko waliouawa na tauni . . . na vita vyote vya karne ya ishirini.”
-