-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Katika 1930, kulikuwa Mashahidi wa Yehova kama mia moja tu katika sehemu yote ya kusini mwa Afrika. Hata hivyo, walikuwa na mgawo uliotia ndani karibu Afrika yote kusini mwa ikweta na baadhi ya maeneo yaliyoenea kaskazini mwa ikweta. Kueneza eneo lenye mweneo mkubwa sana kadiri hiyo kwa ujumbe wa Ufalme kulitaka mapainia halisi. Frank na Gray Smith walikuwa wa aina hiyo.
Walisafiri kwa meli kilometa 4,800 mashariki na kaskazini kutoka Cape Town na kisha wakaendelea kwa gari muda wa siku nne katika barabara mbovumbovu ili wafike Nairobi, Kenya (katika Afrika Mashariki ya Uingereza). Katika muda uliopungua mwezi mmoja, waliangusha vibweta 40 vya fasihi ya Biblia. Lakini, kwa kusikitisha, wakiwa katika safari yao ya kurudi, Frank akafa kwa maleria.
-
-
Sehemu ya 2—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Ramani/Picha katika ukurasa wa 435]
Mapainia wenye bidii kama vile Frank Smith na ndugu yake Gray (anayeonyeshwa katika picha iliyo upande wa juu) walieneza habari njema katika pwani ya mashariki ya Afrika
[Ramani]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
UGANDA
KENYA
TANZANIA
AFRIKA KUSINI
-