-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na yeye akafungua shimo la abiso, na moshi ukapaa kutoka shimo kama moshi wa tanuri kubwa, na jua likatiwa giza, pia hewa, kwa moshi wa shimo lile. Na katika moshi wakatoka nzige wakaenda juu ya dunia; na mamlaka walipewa wao, mamlaka ile ile kama ambayo nge wa dunia wanayo.” (Ufunuo 9:2, 3, NW)
-
-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
8. Inakuwaje kwamba kuachiliwa kwa wale nzige kunaandamana na “moshi” mwingi?
8 Yohana anapotazama, kuachiliwa kwa nzige kunaandamana na moshi mwingi, kama “moshi wa tanuri kubwa.”c Ndivyo ilivyothibitika kuwa katika 1919. Hali ilikuwa yenye giza kwa Jumuiya ya Wakristo na kwa ulimwengu kwa ujumla. (Linga Yoeli 2:30, 31.) Kuachiliwa kwa hao nzige wa jamii ya Yohana kulikuwa ushinde kikweli kwa viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo, ambao walikuwa wametunga hila ya kuua kabisa kazi ya Ufalme na ambao sasa walikataa Ufalme wa Mungu. Ithibati ya giza lenye kufunika kama moshi ilianza kuenea juu ya Jumuiya ya Wakristo yenye kuasi imani wakati hicho kikosi cha nzige kilipopewa mamlaka na kikaanza kuitumia katika kupiga mbiu ya jumbe za hukumu zenye kujaa nguvu. “Jua” la Jumuiya ya Wakristo mwonekano wayo wa kuwa mtio-nuru—lilipatwa na giza, na “hewa” ikawa nzito kwa majulisho-wazi ya hukumu za kimungu wakati “mtawala wa mamlaka ya hewa” alipoonyeshwa kuwa ndiye mungu wa Jumuiya ya Wakristo.—Waefeso 2:2, NW; Yohana 12:31; 1 Yohana 5:19.
-