-
“Waweza Kuacha—Sisi Tuliacha!”Amkeni!—1998 | Desemba 8
-
-
Kulingana na masimulizi fulani, meli za Ulaya zilizotia nanga Japani miaka ya mwisho-mwisho ya 1500 zilibeba wageni waliokuwa wakivuta sigareti, ambao walionekana kana kwamba “wanachochea moto ndani ya tumbo.” Mshangao huo ukawa udadisi, hivi kwamba kufikia miaka ya 1880, zoea la tumbaku lilikuwa limekuwa la kawaida katika Japani. Ni nani ambaye angefikiria kwamba wazao wa Wajapani hao waliokuwa wameshangaa leo wangekuwa miongoni mwa wavutaji wakubwa zaidi wa sigareti ulimwenguni?
-
-
“Waweza Kuacha—Sisi Tuliacha!”Amkeni!—1998 | Desemba 8
-
-
Tumbaku Leo
Karibu asilimia 56 ya wanaume Wajapani huvuta sigareti, wakilinganishwa na asilimia 28 tu ya wanaume Wamarekani walio na umri wa miaka 15 au zaidi. Wavutaji-sigareti wa Japani wapatao 34,000,000 wanatia ndani asimilia 22 ya wanawake, wengi wao wakiwa vijana. Vielelezo vya watu wazima na matangazo ya werevu yamechangia sana ongezeko la haraka la vijana wavutaji-sigareti. Matangazo ya sigareti kwenye televisheni na redio, ambayo yalipigwa marufuku Marekani zaidi ya miongo miwili iliyopita, sasa yamepigwa marufuku Japani.
Zaidi ya hilo, sigareti hupatikana kwa urahisi katika mashine nyingi za kuuzia za pembeni za barabara za Japani. Mara washikapo pakiti hiyo mkononi, ni wachache tu ambao hutii ujumbe dhaifu na wa kijuu-juu tu uliochapwa juu yake. Huenda kibandiko kikasema tu: “Tusivute sigareti sana; inaweza kudhuru.” Na kuongezea uhakika wa kwamba hatari mbaya za tumbaku mara nyingi huendelea, kielelezo kibaya cha watu wengi mashuhuri pia hutia moyo Wajapani wavute sigareti, ikiwahadaa kuwa wana aina fulani ya usalama.
Si ajabu, kwamba wapinzani wa uvutaji-sigareti hulaumu uzembe wa Japani wa kutofanya raia wake wengi waache kutumia tumbaku. Lakini waelimishaji wanaanza kuona umaana na kuonya watu kwamba kuvuta sigareti huhatarisha afya yao na uhai wao. Naam, wavutaji-sigareti Wajapani hupatwa na magonjwa yaleyale kama wavutaji-sigareti kwingineko—kichefuchefu, kutopumua vizuri, kukohoa daima, kuumwa na tumbo, kupoteza hamu ya kula, kushikwa na homa kwa urahisi, na labda baada ya muda fulani, kifo cha mapema kutokana na kansa ya mapafu, maradhi ya moyo, au matatizo mengineyo.
Tangu Aprili 1, 1985, utengenezaji wa tumbaku nchini Japani ulifanywa uwe biashara ya kibinafsi, ikikomesha miongo kadhaa ya kudhibitiwa na serikali. Hata hivyo, bado huo hufurahia uhusiano wa karibu na serikali ambao huzuia hatua zozote kubwa za kukataza kuvuta sigareti. Hiyo ndiyo sababu vikundi vya kupinga tumbaku huona Japani leo kuwa mahali salama pa wavutaji-sigareti. Na yaonyesha sababu inayofanya The Daily Yomiuri liripoti kwamba madaktari hapa wanasikitikia kwamba Japani “ni jamii inayotia moyo uvutaji-sigareti.”
-