-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na maiti zao zitakuwa katika njia pana ya jiji kubwa ambalo kwa maana ya kiroho huitwa Sodoma na Misri, ambako pia Bwana yao alitundikwa kwenye nguzo.
-
-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Lakini hili “jiji kubwa” lilikuwa nini?
22. (a) Ni nini jiji kubwa? (b) Vichapo vya umma vilijiungaje na viongozi wa kidini katika kushangilia juu ya kunyamazishwa kwa mashahidi wawili? (Ona kisanduku.)
22 Yohana anatupa sisi madokezo fulani. Yeye anasema kwamba Yesu alitundikwa kwenye nguzo huko. Hivyo mara moja sisi tunafikiria Yerusalemu. Lakini yeye anasema pia kwamba hilo jiji kubwa linaitwa Sodoma na Misri. Basi, Yerusalemu halisi liliitwa Sodoma wakati mmoja kwa sababu ya mazoea yalo machafu. (Isaya 1:8-10; linga Ezekieli 16:49, 53-58.) Na Misri, ile serikali ya ulimwengu kubwa ya kwanza, nyakati nyingine huonekana ikiwa picha ya huu mfumo wa mambo wa ulimwengu. (Isaya 19:1, 19; Yoeli 3:19) Kwa sababu hiyo, jiji hili kubwa ni picha ya “Yerusalemu” lililochafuliwa ambalo hudai kuabudu Mungu lakini ambalo limekuwa chafu na lenye dhambi, kama Sodoma, na sehemu ya huu mfumo wa wambo wa ulimwengu wa kishetani, kama Misri. Ni picha ya Jumuiya ya Wakristo, ambayo ni kisawe cha Yerusalemu lisilo jaminifu, tengenezo ambalo washiriki walo walikuwa na sababu kubwa sana ya kushangilia wakati waliponyamazisha ile kazi sumbufu ya mashahidi wawili ya kuhubiri.
-
-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na katika saa hiyo likatukia tetemeko la dunia kubwa, na asilikumi ya jiji ikaanguka; na watu elfu saba wakauawa na hilo tetemeko la dunia, na wanaobaki wakashikwa na kikuli na wakampa Mungu wa mbingu utukufu.” (Ufunuo 11:13, NW) Kulikuwako vurugu kubwa kikweli katika milki ya dini. Ardhi ilionekana inajongeza chini ya viongozi wa makanisa yaliyoimarishwa wakati hiki kikundi cha Wakristo kilichohuishwa kilipoanza kufanya kazi. Asilikumi moja ya jiji lao, kitamathali watu 7,000, waliathiriwa sana sana hivi kwamba wanasemekana kuwa waliuawa.
26. Ni nani wanaowakilishwa na “asilikumi ya jiji” na “elfu saba” wa Ufunuo 11:13? Fafanua.
26 Usemi “asilikumi ya jiji” hukumbusha sisi kwamba Isaya alitoa unabii kwa habari ya Yerusalemu la kale kwamba asilikumi ingeokoka uharibifu wa jiji hilo ikiwa mbegu takatifu. (Isaya 6:13) Hali kadhalika, nambari 7,000 hutukumbusha kwamba wakati Eliya alipohisi kwamba ni yeye pekee aliyebaki akiwa mwaminifu katika Israeli, Yehova alimwambia kwamba kwa uhakika kungali kulikuwako 7,000 ambao hawakuwa wameinamia Baali. (1 Wafalme 19:14, 18) Katika karne ya kwanza, mtume Paulo alisema kwamba hao 7,000 walikuwa ni picha ya baki la Wayahudi ambalo lilikuwa limeitikia habari njema juu ya Kristo. (Warumi 11:1-5) Maandiko haya hutusaidia sisi kuelewa kwamba “elfu saba” na “asilikumi ya jiji” katika Ufunuo 11:13 ni wale ambao huitikia mashahidi wawili waliorudishwa na ambao wanaacha jiji kubwa lenye dhambi. Wao ni kana kwamba wanakufa kwa Jumuiya ya Wakristo. Majina yao huondolewa kutoka katika orodha za umemba. Kwa kadiri inavyohusika wao hawaishi tena.d
-