-
Je, “Hekima ya Kutoka Juu” Inakuongoza Maishani?Mkaribie Yehova
-
-
Sura ya 22
Je, “Hekima ya Kutoka Juu” Inakuongoza Maishani?
1-3. (a) Solomoni alionyeshaje hekima ya pekee katika kuamua ni nani aliyekuwa mama ya mtoto? (b) Yehova anaahidi kutupatia nini, na ni maswali gani yanayozuka?
ILIKUWA kesi ngumu sana—wanawake wawili walibishania mtoto mmoja mchanga. Wanawake hao waliishi pamoja, na mmoja wao alijifungua mwana siku chache tu baada ya mwingine kujifungua. Mtoto mmoja alikuwa amekufa, na kila mwanamke alidai kwamba mtoto aliyekuwa hai alikuwa wake.a Hapakuwa na watu wengine walioshuhudia lililotukia. Yaelekea kwamba kesi hiyo ilikuwa imesikilizwa katika mahakama ya chini lakini haikusuluhishwa. Mwishowe, kesi hiyo ilipelekwa kwa Solomoni, mfalme wa Israeli. Je, angefunua ukweli wa mambo?
2 Baada ya kuwasikiliza wanawake hao wakibishana kwa muda, Solomoni aliomba upanga. Kisha, akaamuru mtoto huyo akatwe vipande viwili na kila mwanamke apewe kipande kimoja. Mara moja mama ya mtoto huyo akamsihi mfalme amkabidhi yule mwanamke mwingine mtoto wake mpendwa. Lakini mwanamke yule mwingine aliendelea kusisitiza mtoto huyo akatwe vipande viwili. Sasa Solomoni akajua ukweli wa mambo. Alijua jinsi ambavyo mama humhurumia na kumpenda sana mtoto wake, naye alitumia ujuzi huo kutatua kesi hiyo. Hebu wazia furaha ya mama huyo Solomoni alipompa mtoto wake na kusema: “Yeye ndiye mama yake.”—1 Wafalme 3:16-27.
3 Solomoni alikuwa na hekima ya pekee, sivyo? Watu walistaajabu sana waliposikia jinsi Solomoni alivyosuluhisha kesi hiyo, “maana waliona ya kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake.” Naam, hekima ya Solomoni ilikuwa zawadi kutoka kwa Mungu. Yehova alikuwa amempa “moyo wa hekima na wa akili.” (1 Wafalme 3:12, 28)
-
-
Je, “Hekima ya Kutoka Juu” Inakuongoza Maishani?Mkaribie Yehova
-
-
a Andiko la 1 Wafalme 3:16 linasema kwamba wanawake hao walikuwa makahaba. Kichapo Insight on the Scriptures chasema: “Huenda wanawake hao hawakuwa makahaba wa kulipwa bali walikuwa wamefanya uasherati. Labda walikuwa wanawake Wayahudi au wanawake wa kigeni.”—Kilichochapishwa na Mashahidi wa Yehova.
-