-
Faraja kwa WalioonewaMnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
-
-
Katika Biblia, Zaburi 72 husema juu ya mfariji mtukufu wa watu wote. Zaburi hiyo iliandikwa na baba ya Sulemani, Mfalme Daudi. Maandishi yayo ya utangulizi yasomeka hivi: “Kuhusu Sulemani.” (NW) Yaonekana, iliandikwa na Mfalme Daudi aliyezeeka kuhusu Yule ambaye angekirithi kiti chake cha ufalme. Huyo, kulingana na hiyo zaburi, angeleta kitulizo cha kudumu kutoka katika uonevu. “Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma. Na awe na enzi toka bahari hata bahari, . . . hata miisho ya dunia.”—Zaburi 72:7, 8.
Yamkini, Daudi alipoandika maneno hayo, alikuwa akimfikiria mwana wake Sulemani. Lakini Sulemani alitambua kuwa asingeweza kuwatumikia wanadamu kwa njia iliyofafanuliwa katika hiyo zaburi. Angeweza kutimiza maneno ya hiyo zaburi kwa njia ndogo tu na kwa niaba ya taifa la Israeli, wala si kwa faida ya dunia nzima. Yaonekana, zaburi hiyo ya kiunabii iliyopuliziwa ilielekezea mtu mkubwa zaidi kuliko Sulemani. Huyo alikuwa nani? Angeweza tu kuwa Yesu Kristo.
Malaika alipotangaza kuzaliwa kwa Yesu, alisema hivi: “Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.” (Luka 1:32) Tena, Yesu alijirejezea kuwa “mkubwa kuliko Sulemani.” (Luka 11:31) Tangu ufufuo wa Yesu kwenye mkono wa kuume wa Mungu, amekuwa mbinguni, mahali ambapo akiwa hapo aweza kutimiza maneno ya Zaburi 72. Zaidi, amepokea nguvu na mamlaka kutoka kwa Mungu ya kuvunja nira ya wanadamu waonevu. (Zaburi 2:7-9; Danieli 2:44) Kwa hiyo Yesu ndiye atakayetimiza maneno ya Zaburi 72.
-
-
Faraja kwa WalioonewaMnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 1
-
-
Ili kupata jibu la swali hilo, acheni tusome maneno haya ya ziada ya Zaburi 72 ambayo yatatimizwa katika Kristo Yesu: “Atamkomboa mhitaji aliapo, na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi. Atamhurumia aliye dhaifu na maskini, na nafsi za wahitaji ataziokoa. Atawakomboa nafsi zao na kuonewa na udhalimu, na damu yao ina thamani machoni pake.” (Zaburi 72:12-14) Hivyo Mfalme aliyewekwa rasmi wa Mungu, Yesu Kristo, atahakikisha kwamba hakuna atesekaye kwa sababu ya uonevu. Yeye ana nguvu za kumaliza aina zote za ukosefu wa haki.
-