-
Hekalu Kubwa la Kiroho la YehovaMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
-
-
Pia, kupitia ubatizo wake kwa maji na roho takatifu, yule mwanamume Yesu Kristo alizaliwa mara ya pili akiwa Mwana wa kiroho wa Mungu. (Linganisha Yohana 3:3.) Hilo lilimaanisha kwamba kwa wakati ufaao Mungu angemrudisha Mwanaye kwenye uhai wa kimbingu, ambapo angetumikia kwenye mkono wa kuume wa Babaye akiwa Mfalme na Kuhani wa Cheo cha Juu “hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.”—Waebrania 6:20; Zaburi 110:1, 4.
-
-
Hekalu Kubwa la Kiroho la YehovaMnara wa Mlinzi—1996 | Julai 1
-
-
13, 14. (a) Patakatifu pa hekalu hufananisha nini katika kisa cha Yesu na wafuasi wake watiwa-mafuta? (b) Kinara cha dhahabu hufananisha nini?
13 Chumba cha kwanza cha hekalu hufananisha hali iliyo bora zaidi kuliko ile ya ua. Katika kisa cha mwanadamu mkamilifu Yesu Kristo, hicho hufananisha kuzaliwa kwake tena akiwa Mwana wa kiroho wa Mungu mwenye taraja la kurudia uhai wa kimbingu.
-