Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Ugonjwa Hatari Ambao Umeenea Zaidi Katika Historia Yote”
    Amkeni!—2002 | Novemba 8
    • Kati ya nchi zote ulimwenguni, nchi ya Afrika Kusini ndiyo ina idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa. Inakadiriwa kwamba watu milioni 4.7 wameambukizwa. Katika nchi hiyo, watoto 5,000 huzaliwa na virusi vya UKIMWI kila mwezi. Alipokuwa akihutubia Kongamano la 13 la Kimataifa Kuhusu UKIMWI lililofanywa huko Durban mwezi wa Julai 2000, Nelson Mandela, Rais wa zamani wa Afrika Kusini alisema hivi: “Tulishtuka kugundua kwamba nusu ya vijana wa Afrika Kusini watakufa kutokana na UKIMWI. Jambo lenye kutia hofu hata zaidi ni kwamba maambukizo yote hayo, na mateso yanayosababishwa nayo . . . yangeweza na yanaweza kuzuiwa.”

  • UKIMWI Waenea Katika Afrika
    Amkeni!—2002 | Novemba 8
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 5]

      DAWA YA UKIMWI YA NEVIRAPINE NA TATIZO LINALOKUMBA AFRIKA KUSINI

      Dawa ya Nevirapine ni nini? Kulingana na Nicole Itano, ambaye ni mwandishi wa habari, hiyo ni “dawa ya kuzuia utendaji wa virusi ambayo imejaribiwa na ikaonekana kwamba inaweza kupunguza kwa asilimia 50 uwezekano wa mama kumwambukiza mtoto wake UKIMWI.” Kampuni moja ya kutengeneza dawa huko Ujerumani ilijitolea kuipatia nchi ya Afrika Kusini dawa hiyo bila malipo kwa miaka mitano ijayo. Hata hivyo, kufikia Agosti 2001, serikali haikuwa imekubali msaada huo. Tatizo ni nini?

      Watu milioni 4.7 wana virusi vya UKIMWI nchini Afrika Kusini. Hiyo ndiyo idadi kubwa zaidi ulimwenguni pote. Mnamo Februari 2002, gazeti la The Economist la London liliripoti kwamba Rais Thabo Mbeki wa Afrika Kusini “anashuku yale maoni ya kawaida kwamba virusi vya HIV husababisha UKIMWI” na pia “ana shaka kuhusu gharama za dawa zinazozuia utendaji wa virusi vya UKIMWI, athari zake, na ikiwa zinafanya kazi. Hajazipiga marufuku, lakini madaktari wa Afrika Kusini wanavunjwa moyo wasizitumie.” Kwa nini jambo hilo linasababisha hangaiko kubwa? Kwa sababu kila mwaka maelfu ya watoto huzaliwa na virusi vya UKIMWI huko Afrika Kusini na asilimia 25 ya wanawake wajawazito wana virusi hivyo.

      Kwa sababu ya maoni hayo yanayotofautiana, kesi iliwasilishwa mahakamani ili kuilazimisha serikali igawe dawa ya nevirapine. Mahakama ya Sheria ya Afrika Kusini ilitoa uamuzi wake mnamo Aprili 2002. Kulingana na taarifa ambayo Ravi Nessman aliandika katika gazeti la The Washington Post, mahakama hiyo iliamua kwamba “serikali inapaswa kuruhusu dawa hiyo katika taasisi za matibabu ambazo zinaweza kuigawa kwa njia inayofaa.” Ijapokuwa serikali ya Afrika Kusini ilikuwa ikigawanya dawa hiyo katika vituo 18 vya majaribio nchini humo, inasemekana kwamba uamuzi huo umewapa tumaini wanawake wote wajawazito wenye virusi vya UKIMWI katika nchi hiyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki