Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mtumishi mmoja wa akina ndugu aliyewekwa rasmi mwaka wa 1943 ni Gert Nel, aliyejifunza kweli mwaka wa 1934 akiwa mwalimu katika shule moja huko Northern Transvaal. Aliwasaidia wahubiri wengi na bado wengi wanakumbuka utumishi wake wa uaminifu. Alikuwa mrefu na mwembamba na alionekana kuwa mkali, naye alipigania kweli kwa bidii. Alikuwa na kumbukumbu nzuri sana na pia aliwapenda watu sana. Alikuwa akihubiri kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja au mbili jioni bila kupumzika. Katika safari zake akiwa mwangalizi anayesafiri, alikuwa anapanda gari-moshi wakati wowote iwe mchana au usiku; anatembelea kutaniko moja kwa siku kadhaa ikitegemea ukubwa wa kutaniko hilo; kisha anaenda kutaniko linalofuata. Ndivyo alivyofanya juma baada ya juma. Alialikwa Betheli mwaka wa 1946 awe mtafsiri wa Kiafrikana, naye aliendelea kutumikia huko kwa uaminifu hadi alipokufa mwaka wa 1991. Ndiye ndugu mtiwa-mafuta wa mwisho kutumikia Betheli ya Afrika Kusini.

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 95]

      Gert Nel, mtumishi wa akina ndugu, 1943

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki