Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Makutaniko na watu binafsi walituma barua nyingi kwa ofisi ya tawi ya Afrika Kusini kusimulia utimilifu wa ndugu weusi. Barua moja kama hiyo iliandikwa na mzee wa kutaniko fulani huko KwaZulu-Natal. Ilisema hivi: “Tunawaandikia barua hii kuwajulisha kwamba tumempoteza ndugu yetu mpendwa Moses Nyamussua. Alikuwa fundi wa vyuma na magari. Wakati mmoja, washiriki wa kundi la kisiasa walimwomba amalizie kuunda bunduki walizokuwa wamejitengenezea, naye akakataa. Kisha, Februari 16, 1992, kundi hilo lilifanya mkutano wa kisiasa, ambako vita vilizuka kati ya washiriki wake na wale wa kundi pinzani. Jioni ya siku hiyohiyo, walipokuwa wakirudi kutoka kupigana, walikutana na ndugu huyo akienda madukani. Walimuua papo hapo kwa mikuki yao. Kwa nini? Walisema: ‘Ulikataa kutuundia bunduki, na sasa wenzetu wameuawa vitani.’ Kisa hicho kimewashtua sana akina ndugu, lakini tutaendelea kutimiza huduma yetu.”

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 122]

      Moses Nyamussua aliuawa na umati

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki