-
Afrika Kusini2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
WAPIGANIA KWELI BILA WOGA
Katika miaka hiyo ya mapema, kikosi hicho kidogo cha wahubiri kiliitetea kweli bila woga. Huko Nylstroom, katika mkoa wa Northern Transvaal (ambao leo unaitwa Mkoa wa Limpopo), wanafunzi wawili wavulana walisoma kijitabu What Say the Scriptures About Hell? Walisisimuka sana kujifunza kweli kuhusu wafu. Mmoja wao, Paul Smit,a alisema hivi: “Nylstroom pakawa kituo cha vurugu, kana kwamba pamekumbwa na tufani, wakati ambapo sisi wanafunzi wawili tulipotangaza waziwazi kwamba mafundisho ya kanisa ni ya uwongo. Punde si punde, watu mbalimbali walikuwa wakizungumza kuhusu dini hiyo mpya. Bila shaka, kama ilivyo kawaida yao, makasisi walisema uwongo kuhusu watu wa Mungu na kuwatesa. Kwa miezi kadhaa, hata miaka, mahubiri yao ya kila juma yalikuwa juu ya kitu kimoja tu, eti ‘dini ya uwongo.’”
-
-
Afrika Kusini2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
a Masimulizi ya maisha ya Paul Smit yalikuwa katika gazeti la Kiingereza la Mnara wa Mlinzi la Novemba (Mwezi wa 11) 1, 1985, ukurasa wa 10-13.
-