Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ivan Klimko anasema hivi: “Wakati mmoja katika Kambi Na. 19 ya Mordvinia, askari wenye mbwa waliwaamuru akina ndugu watoke kambini na wakafanya msako mkali. Kila Shahidi alivuliwa nguo zote, kutia ndani matambara aliyokuwa amevaa miguuni. Lakini akina ndugu walibandika kwa gundi karatasi zilizonakiliwa kwa mkono chini ya nyayo za miguu, na hivyo karatasi hizo hazikugunduliwa. Pia walitengeneza vijitabu vidogo ambavyo vingeweza kutoshea katikati ya vidole. Walinzi walipowaamuru watu wote wainue mikono yao, vijitabu hivyo havikuanguka, na hivyo baadhi ya vichapo hivyo havikupatikana.”

  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ndugu Klimko anakumbuka hivi: “Pindi moja, tulipoteza vichapo vingi na hata Biblia. Vichapo hivyo vilikuwa vimefichwa katika mguu wa bandia wa ndugu mmoja. Baada ya kumlazimisha ndugu huyo atoe mguu wake, walinzi waliuvunja. Kisha walipiga picha kurasa zilizotawanyika na kuzichapisha kwenye gazeti la gereza hilo. Hata hivyo, hilo lilikuwa jambo zuri kwani lilionyesha kwamba Mashahidi wa Yehova walijihusisha katika utendaji wa kidini tu. Baada ya ugunduzi huo, msimamizi wa kambi aliwaambia akina ndugu hivi kwa kejeli, ‘Hii ndiyo Har–Magedoni yenu!’ Hata hivyo, siku iliyofuata, mtu fulani alimwambia kwamba Mashahidi wa Yehova wamekutana, wakaimba nyimbo, na kusoma kama ilivyo kawaida yao.”

  • Urusi
    2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 173]

      Ivan Klimko

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki