Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Waumini Wako Wapi?
    Amkeni!—1996 | Aprili 8
    • KWENYE uwanda wenye upepo mkali katika eneo la kaskazini mwa Hispania upo mji mdogo wa Caleruega. Mji huo wa enzi za kati umedhibitiwa na makao ya watawa yenye kupendeza yaliyojengwa kwa mtindo wa Kiitalia. Yalijengwa miaka 700 iliyopita kwa kumheshimu Domingo de Guzmán, mwanzilishi wa utaratibu wa watawa wa kiume, ambaye alizaliwa hapa. Kwa karne saba makao hayo ya watawa yalikaa watawa wa kike ambao huchagua kuishi katika ukimya na kujitenga.

      Paa la makao hayo ya watawa lavuja, na kuta za kale zimeanza kuporomoka. Lakini mama-mkuu anahangaikia kuzorota kuovu zaidi—kuporomoka kwa dini yenyewe. “Nilipoingia katika makao haya ya watawa miaka 30 iliyopita, kulikuwa na watawa wa kike 40 hapa,” yeye aeleza. “Sasa tuko 16 tu. Hakuna wachanga. Wito wa kimungu wa maisha ya kidini waonekana umekuwa jambo lililopita.”

  • Waumini Wako Wapi?
    Amkeni!—1996 | Aprili 8
    • Katika miaka 25 ambayo imepita, asilimia ya Wahispania ambao hujiona kuwa “Wakatoliki watendaji” imeshuka kutoka asilimia 83 hadi asilimia 31. Katika 1992, askofu mkuu Mhispania Ramon Torrella aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba “Hispania ya Kikatoliki haipo; watu huenda kwenye maandamano ya Juma Takatifu na Misa ya Krismasi—lakini si [kwenye Misa] ya kila juma.” Wakati wa ziara ya papa huko Madrid katika 1993, John Paul 2 alionya kwamba “Hispania yahitaji kurudi kwenye mizizi yayo ya Kikristo.”

  • Waumini Wako Wapi?
    Amkeni!—1996 | Aprili 8
    • Hispania kukiwa na wapatao 8,000 ambao wameacha ukasisi ili kufunga ndoa.

  • Waumini Wako Wapi?
    Amkeni!—1996 | Aprili 8
    • zaidi ya asilimia 50 ya Wakatoliki Wafaransa, Waitalia, na Wahispania wakiwa hawaamini miujiza.

  • Waumini Wako Wapi?
    Amkeni!—1996 | Aprili 8
    • Katika Hispania, kondomu—ambazo zilikaribia kuwa bidhaa ya magendo miongo miwili iliyopita—hutangazwa kwa ukawaida kwenye televisheni,

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki