-
Jilinde Ili Pepo WasikudhuruMnara wa Mlinzi—2009 | Mei 1
-
-
Kwa mfano, uzinzi na ngono kabla ya ndoa zinashutumiwa katika jamii nyingi na vilevile katika Biblia. (1 Wakorintho 6:9, 10) Hata hivyo, katika baadhi ya jamii za eneo la Pasifiki, mazoea kama hayo yanakubalika msichana akisema kwamba “amerogwa kwa jani la kijani kibichi,”a yaani, akisema kwamba alilazimika kufanya ngono kwa sababu amerogwa.
Hata hivyo, Biblia inafundisha kwamba sisi tutatozwa hesabu kwa matendo yetu. (Waroma 14:12; Wagalatia 6:7) Kwa mfano, mwanamke wa kwanza, Hawa, alihisi kwamba alishawishiwa na Shetani kumuunga mkono na kutomtii Mungu. Alisema: “Yule nyoka—alinidanganya nami nikala.” Hata hivyo, Yehova alimwadhibu Hawa kupatana na matendo yake. (Mwanzo 3:13, 16, 19) Pia atatutoza hesabu kupatana na matendo yetu.—Waebrania 4:13.
-
-
Jilinde Ili Pepo WasikudhuruMnara wa Mlinzi—2009 | Mei 1
-
-
a Msemo huo unamaanisha kwamba msichana alipewa jani au chakula kilichorogwa. Lile jani au chakula kinadhaniwa kumfanya yule msichana avutiwe na mwanamume fulani. Desturi hii si sawa na kumpa msichana dawa za kulevya bila yeye kujua, kisha kumlazimisha kufanya ngono kinyume cha mapenzi yake. Katika kisa hiki cha pili msichana hana hatia.
-