Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • “Mbwa-mwitu na mwana-kondoo watalisha pamoja, na simba atakula majani kama ng’ombe; na mavumbi yatakuwa chakula cha nyoka. Hawatadhuru wala kuharibu katika mlima wangu mtakatifu wote, asema BWANA.” (Isaya 65:25)

  • ‘Mkashangilie Daima kwa Ajili ya Hivi Niviumbavyo’
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 34. Maneno ya Yehova yana utimizo gani wenye kusisimua leo na katika ulimwengu mpya?

      34 Leo maneno ya Yehova yanatimizwa kwa njia ya kusisimua miongoni mwa waabudu wa kweli. Tangu mwaka wa 1919, Mungu ameibariki nchi ya kiroho ya watu wake, akaigeuza kuwa paradiso ya kiroho. Wale wanaoingia katika paradiso hii ya kiroho hufanya mabadiliko ya ajabu katika maisha yao. (Waefeso 4:22-24) Watu mmoja-mmoja ambao wakati mmoja walikuwa na nyutu za kinyama—ambao labda waliwatumia vibaya wanadamu wenzao au wakawadhulumu kwa njia nyinginezo—wanafanya maendeleo ya kuyamaliza makali ya tabia zisizopendeza kwa msaada wa roho ya Mungu. Matokeo ni kwamba, wanafurahia amani na umoja wa ibada pamoja na waamini wenzao. Baraka zinazofurahiwa sasa na watu wa Yehova katika paradiso yao ya kiroho zitaendelea mpaka ndani ya Paradiso halisi, ambamo amani itakuwamo miongoni mwa wanadamu, na hali kadhalika miongoni mwa wanyama.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki