Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Sri Lanka: Mawimbi yalikumba thuluthi mbili za pwani ya kisiwa hicho na kusababisha uharibifu mkubwa. Mawimbi hayo ya tsunami yalitokea Jumapili asubuhi wakati ndugu wengi walipokuwa mikutanoni katika eneo ambalo halikuathiriwa. Makutaniko kumi yaliathiriwa na dada mmoja akafa pale nyumba yake ilipobebwa na maji hadi baharini. Akina ndugu wanaomboleza sana kifo cha dada huyo mzuri. Watu fulani wanaopendezwa walikufa na ndugu wengi walifiwa na watu wa ukoo. Mzee mmoja wa kutaniko alifiwa na watu 27 wa jamaa yake! Licha ya hayo, “akina ndugu wameokoka msiba huo bila kupatwa na dhara lolote la kiroho,” ofisi ya tawi inaandika.

      Misaada mingi sana ilimiminika Betheli nao Wanabetheli wengi wakasaidia kuigawa. Magari ya akina ndugu yalitumiwa kusafirisha misaada hiyo kwenye maeneo yaliyoathiriwa. Ilichukua siku nne tu kuwapata ndugu wote na kuwapa chakula na mavazi. Walipoulizwa wanataka nini kingine, walijibu: “Biblia na vitabu! Vitabu vyetu vilibebwa na maji.” Walipewa vitu hivyo mara moja.

      Mwangalizi wa mzunguko Gerrad Cooke, alikuwa Colombo wakati huo. Gerrad alisafiri kwa gari lake kwa muda wa saa saba kwenye barabara ambayo ni hatari usiku kwa sababu ya tembo. Alipowasili mwendo wa saa 4:30 usiku, yeye pamoja na ndugu mwingine wa eneo hilo, ambaye nyumba yake ilikuwa imejaa maji, walianza kutembelea familia za akina ndugu na kuwapa misaada. Walifanya kazi hiyo mpaka che.

  • Matukio Muhimu ya Mwaka Uliopita
    2006 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 24]

      Misaada yashughulikiwa nchini Sri Lanka

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki