-
Upendo UnaoshikamanishaAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Karne nyingi zilizopita kulikuwa na meli nyingine katika dhoruba kali mno. Mtume Paulo na wengine 275 walikuwa melini. Wakihofia kwamba meli hiyo ingevunjika vipande-vipande kutokana na ukali wa dhoruba hiyo, yaelekea mabaharia hao walipitisha “misaada”—minyororo au kamba—chini ya meli kutoka upande mmoja hadi mwingine ili kushikanisha pamoja vipande vya mbao vilivyofanyiza sehemu za nje za meli hii ya kibiashara. Abiria wote waliokuwamo walisalimika, ingawa meli hiyo haikusalimika.—Matendo, sura 27.
-
-
Upendo UnaoshikamanishaAmkeni!—1996 | Oktoba 8
-
-
Katika siku ya Paulo, meli ilipokabili dhoruba kali, kusalimika kwa abiria na meli kulitegemea ustadi wa wafanyakazi wa melini na vilevile jinsi meli hiyo imeshikamanishwa pamoja. Ilikuwa hivyo pia katika maana ya kitamathali. Ingawa Paulo alikuwa amestahimili unyimivu wa kimwili, kufungwa gerezani, na kuteswa, dhoruba kali kupita zote ambayo ilitahini uthabiti na uwezo wake wa kiroho na kihisia-moyo wa kuendelea kupenda, ilikuja kutoka ndani ya kutaniko la Kikristo.
-